Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
BENKI
ya DCB imezindua utaratibu mpya kwa wateja wake wa kutoa maoni kwa
kutumia mashine ya Happy or not katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa
mteja.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha Mikakati na Ubunifu- DCB,
Samwel Dyamo amesema kuwa huduma hii mpya itasaidia kupata taarifa kwa
mapema zaidi kwani zitakuwa ni kwa njia ya mtandao na zitatoa mrejesho
kwa kampuni ili kuzidi kuboresha zaidi.
Dyamo
amesema, kwa sasa wateja wetu watatumia mashine hiyi badala ya kutumia
boksi la maoni kwani ni njia rahisi sana kuweza kuwafikia wao kwa mapema
kwanj mrejesho utakuja haraka zaidi na mapema.
Kwa
pamoja benki ya DCB waliweza kukata keki na kusherehekea na wateja wao
huku baadhi wakisifia huduma nzuri zinazotolewa na wanapata mikopo kwa
njia rahisi sana na kwa riba nafuu.
Fatma
Simba, amesifia huduma za benki ya DCB na kusema kuwa wanatoa mikopo kwa
urahisi sana ndani ya siku tatu kuanzia kima cha 50,000.
Wiki
ya huduma kwa mteja inaadhimishwa dunia nzima kwa makampuni mbalimbali
na taasisi, ambapo Benki ya DCB wamekuja na kauli mbiu ya Wewe ni
mhimili wetu, tupo kwa ajili yako.
Mkuu
wa Kitengo cha Mikakati na Ubunifu DCB, Samwel Dyamo akizindua kwa
kubonyeza kutufe katika mashine ya Happy or Not jijini Dar es Salaam leo
wakati wa uzinduzi wa mashine hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa kampuni ya Mind Source, Abubakar Faraji akielezea namna ya
kuitumia mashine ya Happy or Not kwa wateja wa Benki ya DCB leo Jijini
Dar es salaam kwenye wiki ya Huduma kwa Mteja.
Wateja na wafanyakazi wa DCB Benki wakiwa wanashuhudia kukata kwa keki sambamba na wateja hao kukata keki.
Mkurugenzi
wa Kitengo cha Mikakati na Uhakiki wa beki ya DCB, Samwel Dyamo
akizungumza na wateja wao katika wiki ya Huduma kwa Mteja leo Jijini Dar
es salaam.
Wafanyakazi
wa Benki ya DCB wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Kitengo cha
Mikakati na Ubunifu Samwel Dyamo katika maadhimisho ya wiki ya Huduma
kwa Mteja tawi la Magomeni.
Tawi
la Benjamin mkapa wakisheherekea wiki ya huduma kwa wateja pamoja na
wateja wao. Sambamba Meneja wa tawi hilo Badru Lashku.
EmoticonEmoticon