Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Makazi, William Lukuvi akisalimia na DAS wa wilaya
ya Ilala Edward Mpogolo, alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya
Kinyerezi Sokoni, kufuatia mgogoro wa wananchi wawili kumilishwa eneo
hilo la makaburi lenye ukubwa wa zaidi ya ekari moja. Katika
sakata hilo, Waziri Lukuvi ameagiza kufutwa kwa umiliki huo mara moja
ifikapo leo jioni, na pia kugiza kusakwa Pascal Kyonya Kazungu na
Ntitonda Chukilizo waliomilikishwa eneo hilo watafutwe na kufikishwa
ofisini kwake kesho
Kadhalika amemwagiza Kaimu Mkurugenzi wa Ardhi mkoa wa Dar es Salaam,
Leo Komba, kuorodhesha majina ya maofisa ardhi wote walioshiriki
kuwamilikisha ardhi hiyo ya eneo la makaburi ili aweze kuwashughulikia
kwa kuwachukulia hatua za kisheria. Kushoto ni Mbunge wa jimbo la Segerea Bona Kalua
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Makazi William Lukuvi akipatiwa maelezo na Mbunge
wa Segerea Bona Kalua alipowasili kwenye eneo hilo la Makaburi ya
Kinyerezi Sokoni leo. Kushoto ni DAS wa wilaya ya Ilala Edward Mpogolo.
Waziri
Lukuvi akiwa na Diwani wa Kata ya Kinyerezi, Grayson Celestine
alipowasili leo kutatua mgogoro wa kumilikishwa eneo la Makaburi ya
Kinyerezi Sokoni Dar es Salaam,.Kushoto ni Dar wa Wilaya ya Ilala,
Edward Mpogolo
Waziri Lukuvi akihoji jambo kwa uongozi wa Kata ya Kinyerezi alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, leo
Waziri
Lukuvi akipata maelezo kutoka kwa uongozi wa Kata ya Kinyerezi
alipowasili kwenye eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni, leo. Kulia ni
Mbunge wa Segerea Bona Kalua
Wananchi wa eneo la Kinyerezi Sokoni wakiwa wamemzunguka Waziri Lukuvi alipowasili kwenye eneo la Makaburi hayo leo
Kaimu
Mkurugenzi wa Ardhi jiji la Dar es Salaam, Leo Komba (kulia) akitoa
maelezo kwa Waziri Lukuvi kuhusu anachofahamu juu ya wananchi wawili
kumilikishwa eneo la Makaburi ya Kinyerezi Sokoni leo
”
Sasa hapo mimi sima la ziada, Wewe si ndiyo Mkurgenzi?” Sawa kuanzia
mda huu, nakuagiza ukafute umilikishwaji ardhi uliofanywa katika eneo la
makaburi haya”, alisema Waziri Lukuvi na kuongeza ” Na wale
waliomilikishwa hapa nitafutieni kesho waje kwangu wanieleze ilikuwaje
hata wakapata kumilikishwa eneo hili, na wale wote walioshiriki kwa
namna yoyote katika kufanya hili uniletee majina yao mara moja”.
Diwani
wa Kata ya Kinyerezi, Grayson Celestine, akimshukuru Waziri wa Ardhi
Nyumba na Makazi, William Lukuvi baada ya kutoa uamuzi wa kufuta
umilikishwaji wa eneo hilo la makaburi kwa watu wawili.
Waziri
Lukuvi akifuatana na DAS wa wilaya ya Ilala wakati akiondoka kwenye
eneo hilo la makaburi ya Kinyerezi, ambako amefanikiwa kumaliza mgogoro
wa wananchi na watu wawili waliokuwa wamemikishwa eneo hilo la Makaburi
ya Kinyerezi Sokoni. Kulia ni Diwani wa Kata ya Kinyerezi Grayson
Celestine. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO
………………………………………………………….
Jonas Kamaleki, MAELEZO
Wakazi wa Kinyerezi Sokoni, Dar
es Salaam wameipongeza Serikali ya awamu ya Tano kwa kufuta hati tatu
zilizokuwazimetolewa katika eneo la makaburi liliouzwa kinyume cha
sheria.
Pongezi hizo zimetolewa leo kwa
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi
baada ya kumwagiza kamishna wa ardhi Kanda ya Dar es Salaam kufuta hati
hizo mara moja na kulirejesha eneo la makaburi kwa wananchi.
Akiongea kwa niaba ya wakazi wa
Kinyerezi, Mwanasheria, Mwinjuma Mzee amesema kuwa Wanakinyerezi
wanamshukuru sana Mhe. Waziri kwa kurejesha eneo la makaburi kwa wakazi
hao.
“Mhe. Waziri na msafara wake wote
tunawashukuru kwa kumaliza mgogogoro huu ambao umedumu kwa muda mrefu
na tumemwomba Waziri ashughulikie na maeneo mengine yanayohusu huduma za
jamii kama zahanati na shule,” alisema Mzee.
Naye mkazi wa Kinyerezi, Bi.
Maimuna Forogo ameelezea furaha yake kwa kumshukuru sana Mhe waziri kwa
hatua aliyoichukua ya kubatilisha hati za umiliki wa makaburi.
“Mimi namnshukuru sana Mhe.
Waziri na Serikali ya awamu ya Tano kwa ujumla kwa kutujali sisi
wananchi, mimi kwenye makaburi haya nilimzika babu yangu sasa wanataka
nimpeleke wapi kwanza ni mifupa mitupu,”alisema Maimuna.
Kwa upande wake, Mhe. Lukuvi
amesema ameamua kubatilisha hati tatu za viwanja zilizotolewa na
watumishi wasiowaaminifu wa Serikali ili eneo hilo liendelee kutumika
kwa ajili ya maziko.
“Nimemuagiza kamishna anitafutie
wahusika ambao walishiriki katika kumilikisha eneo la makaburi kwa watu
ili wachukuliwe hatua za kinidhamu, watu hawa inabidi wafukuzwe kazi
kwani kitendo cha kumilikisha eneo la kuzika hakivumiliki,”alisema
Waziri Lukuvi.
Ameongeza kuwa watu ambao
wanadiriki kuuza makaburi ambayo yametumiwa tangu mwaka 1962 na kwa sasa
yapo zaidi ya 500, ni watu ambao hawana hata hofu ya Mungu hivyo
kufukuzwa ni halali yao.
Mhe. Lukuvi ametoa wito kwa
viongozi wenzake wanapofanya shughuli za mipangomiji nchini kutenga
sehemu za huduma za jamii ikiwemo mahali pa kuzikia kwani kila mtu
atakufa na anahitaji kuzikwa.
“Serikali ya awamu ya Tano tumeamua kurekebisha pote palipokuwa pamepinda ili wananchi wapate haki zao,”alisema Lukuvi.
Aidha amewataka waliokuwa
wamemilikishwa wafike wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili
wampe Waziri uzoefu wanaoutumia kununua maeneo ya huduma za jamii
ikiwemo maeneo ya makaburi ili imsaidie kujua jinsi mtandao ulivyo.
Hati tatu zilizofutwa ni 213, 215 na 217 Kitalu B, Kinyereze, Kata ya Segera jijini Dar es Salaam
EmoticonEmoticon