Mkurugenzi
wa ulinzi na usalama wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa nchi kavu na
majini (Sumatra) Captain Mussa Mandia, katikati akizungumza na
waandishi wa habari mkoani Tanga leo kuzungumzia mpango wa maalumu wa
kupambana na uchafuzi wa mazingira baharini, kushoto ni Meneja
Mawasiliamo wa Sumatra,David Mzirai kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar(ZMA) Suleiman Masoud
Meneja Mawasiliamo wa Sumatra,David Mzirai akisisitiza jambo kwenye
mkutano huo wa leo na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa
Bandari Mkoani Tanga
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Baharini Zanzibar(ZMA) Suleiman Masoud akizungumza katika mkutano huo
Waandishi wa Habari wa Mkoani Tanga wakichukua habari leo
PRO wa Mamlaka ya Bandari Mkoani Tanga (TPA)Moni Jarufu akifuatilia mkutano huo na waandishi wa habari wa mkoani Tanga
…………………………………………………………………..
MAMLAKA
ya udhibiti wa usafiri wa majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imekusudia
kuanzisha mpango mkakati maalumu wa udhibiti uchafuzi wa mazingira
baharini (NMOSCRP) unaosababishwa na umwagaji wa mafuta unaofanywa bila
ya kufuata taratibu za mazingira zilizowekwa na kuharibu mazingira.
Hayo
yalibainishwa leo na Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa vyombo vya
majini Taifa Capt Mussa Hamza wakati akizungumza na waandishi wa habari
kuhusiana na maadhimisho ya siku ya wiki ya bahari dunia inayofanyika
Kitaifa Mkoani Tanga kwenye viwanja vya Tangamano kesho Jumanne.
Ambapo
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa anatarajiwa
kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yatakayokwenda sambamba na
maonyesho mbalimbali na warsha itakayofanyika Septemba 28 mwaka huu.
Alisema
kuwa kutokana na kuwepo kwa biashara ya usafirishaji wa mafuta kwa njia
ya bahari wame lazimika kuanzisha mpango huo ili kukabiliana na
uchafuzi huo ambao unaweza kuchangia utoekaji wa viumbe vya vilivyopo.
Aidha
alisema kuwa kutokana na uchavuzi huo wa mazingira uliopitiliza
unachangia kwa kiasi kikubwa kuhatarisha mazilia ua samaki katika bahari
na viumbe vingine vilivyomo baharini.
Alisema
Tanzania imeingia katika shughuli za uchimbaji wa gesi na mafuta ambapo
usafiri mkubwa wa mafuta ni kwa njia ya bahari hali ambayo inalazimika
kuanzisha sheria maalumu ambayo inaweza kulinda
mazingira ya bahari.
mazingira ya bahari.
“Hakuna
vyombo vinavyokuwa na uwezo wa kubeba mizigo mikubwa kama vyombo bya
baharini hivyo imetulazimu kuanzisha mpango maalumu ambao tunategemea
kesho kuuzindua ili kuweza kukabilia na
uchavuzi wa mazingira katika bahari yetu ya Hindi”Alisema.
uchavuzi wa mazingira katika bahari yetu ya Hindi”Alisema.
Hamza
alitumia fursa hiyo kueleza kuwa miongoni mwa sababu za kufanya
maadhimisho hayo Kitaifa Mkoa wa Tanga ni kutokana na mkoa huo kuingia
katika mradi mkubwa wa usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bomba kutoka
nchini Uganda hadi bandari ya Tanga ambapo kutakuwepo na fursa kubwa ya
kuitangaza Tanga kwa wawekezaji.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya usafirishaji wa Majini
Zanzibar (ZMA) Suleiman Masoud alisema kufanyika kwa maadhimisho hayo
katika mkoa wa Tanga ni tija kwa bandari ya Tanga,kupitia maadhimisho
hayo lengo ni kuitangaza bandari hiyo kwa wafanya biashara wakubwa ndani
na nje ya nchi.
Alisema
Tanga inaweza kuwa ni sehemu kuu ya kitovu cha biashara ya usafirishaji
wa mafuta kwa njia ya bahari na hata nchi kavu ikiwa itawekewa mipango
madhubuti ya kuifufyua bandari ya Tanga.
EmoticonEmoticon