Naibu Waziri wa Nchi ofis ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akiwa na wananchi wa kigamboni waliojitokeza kwaajiri ya kufanya usafi katika fukwe za kigamboni
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina akiongea na waandishi wa habari,hawapo pichani mara baada ya kumaliza kufanya usafi katika fukwe za wilaya ya kigamboni.
EVELYN MKOKOI
AFISA HABARI
OFISI YA MAKAMU WA RAIS
STORY – KIGAMBONI
23/9/2016
Naibu Waziri Ofisi ya
Makamu wa
Rais Muungano na Mazingira Mhe Luhaga Mpina amemtaka Mkuu wa Wilaya
ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa kuhakikisha fukwe zote za kigamboni
zinafanyiwa usafi na kuwa katika hali ya kuridhisha.
Naibu Waziri Mpima ameseyasema
hayo leo katika maeneo ya fukwe za kigamboni aliposhiriki katika siku
ya usafi kitaifa ya mwezi wa September.
Amesema fukwe za kigamboni
ni chafu sana na usafi wa mazingira katika mji wa kigamboni hauridhishi,
“pamoja na wananchi kujitokeza kwa wingi katika kusafisha mazingira
leo fukwe ni chafu na wengine wanatuangalia tunavyosafisha huku wakiendelea
na shughuli zao, Angalia wale wavuvi kwenye mitumbwi yao wanaendelea
na kazi zao na wao ndo wachafuzi wakubwa huko baharini na nchi kavu.
“Alisema.
Mpina amemtaka mkuu
wa wilaya hiyo kuwawajibisha viongozi walioko chini yake kwa kosa la
uzembe wa ufuatiliaji wa sheria ya mazingira kabla hajawajibishwa yeye.
“kiongozi mzembe afukuzwe kazi kabla haujafukuzwa wewe na kuingia
kwenye matatizo.” Alisisitiza naibu waziri Mpina.
Hata hivyo Naibu Waziri
Mpina alimpongeza mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa
kuanzisha kampeni ya upandaji miti maarufu kama ‘’MTI WANGU’’
na kuwashauri wakazi wa jiji kushiriki Katika siku ya uzinduzi na kuahidi
kuwa pamoja nao siku hiyo.
Kwa Upande wake Mkuu
wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa ameelezea jitihada za usafi
wa mazingira katika mji wa kigamboni ikiwa ni pamoja na mashindano ya
usafi wa mazingira na kuwataka wakazi wa kigamboni kuongeza jitihada
za kutosha kuiweka kigamboni safi.
Jumamosi ya Mwisho wa
Mwezi ni siku maalum ya usafi ikiwa ni katika kutekeleza agizo la Rais
la Usafi wa mazingira ambapo mwezi huu kitaifa imefanyika Kigamboni.
EmoticonEmoticon