Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akizungumza
jambo alipofika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera ili kujadiliana
kuhusiana na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa
Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Mstaafu Salim Kijuu.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akielezea jambo wakati
wa kikao na wataalamu wanaofanya utafiti wa tetemeko Mkoani Kagera
(hawapo pichani).
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Profesa Abdulkarim Mruma
ambaye ni kiongozi wa timu ya wataalamu wanaofanya utafiti wa tetemeko
mkoani Kagera akionesha kitovu cha tetemeko hilo katika kijiji cha
Kigazi, Kata ya Minziro kilomita 88 kutoka Bukoba mjini kupitia barabara
ya Bukoba-Kyaka-Minziro.
Baadhi
ya nyumba katika kijiji cha Kampanji kilichopo Mpakani mwa Tanzania na
Uganda ambazo zilibomoka kutokana na tetemeko la ardhi.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akikagua eneo
lililokumbwa na Tetemeko na kusababisha mpasuko kwenye ardhi katika
kijiji cha Kigazi, Kata ya Minziro ndani ya Kitongoji cha Bilongo.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (wa pili kulia)
akizungumza wakati wa ziara ya kukagua shughuli za utafiti wa tetemeko
zinazofanywa na timu wataalamu kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST)
na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kushoto kwake ni Mtendaji Mkuu wa GST,
Profesa Abdulkarim Mruma ambaye ni kiongozi wa timu ya wataalamu hao.
Wataalam
kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) na Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, wanaofanya utafiti wa tetemeko la ardhi lililotokea tarehe 10
Septemba, mwaka huu mkoani Kagera, wametakiwa kuhakikisha kuwa wanafanya
utafiti wa kina ili kubaini namna ambavyo miamba ya maeneo husika
ilivyo na vilevile kuandaa ramani mpya ya miamba katika maeneo
yatakayotafitiwa.
Agizo
hilo limetolewa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
alipofanya ziara mkoani humo kwa lengo la kukagua shughuli za utafiti
wa tetemeko zinazoendelea maeneo mbalimbali mkoani humo.
Alisema
kuwa, utafiti huo utachukua muda mrefu kwani hautafanyika mkoani Kagera
pekee bali utafanyika pia katika Mikoa ya Geita, Mwanza, Shinyanga,
Tabora, Dodoma na baadaye nchi nzima.
Katika
ziara hiyo, Waziri Muhongo aliwaagiza wataalam hao kuhakikisha wanatoa
mafunzo ya awali kwa umma hususan kwenye maeneo yaliyoathiriwa zaidi na
tetemeko ili waelewe nini wanapaswa kufanya endapo tetemeko litatokea.
Aliagiza
elimu hiyo ianze kutolewa siku ya Jumamosi, tarehe 24/9/2016 Saa 4
Asubuhi, huku wakiandaa ratiba ya mafunzo hayo kwa maeneo mengine na
kuandaa vipeperushi vyenye maelezo ya kutosha kuhusu Tetemeko la Ardhi
kwa ajili ya kuwasambazia wananchi.
Aidha,
Profesa Muhongo aliwaagiza wataalam hao, kuepuka kutoa kauli
zinazokinzana ili kuepusha kuwachanganya na kuwaletea hofu wananchi
waliokumbwa na kadhia hiyo na kueleza kuwa Msemaji Mkuu wa wataalam hao
wanaofanya utafiti husika ni Mtendaji Mkuu wa GST, ambaye yupo mkoani
humo akishirikiana na wataalam kufanya utafiti.
Mbali
na hilo, Profesa Muhongo aliagiza kuwa, ujengwe mnara maalum katika eneo
ambalo tetemeko hilo lilianzia huko katika kijiji cha Kigazi, Kata ya
Minziro, kilomita 88 kutoka Bukoba mjini ili iwe kumbukumbu ya baadaye.
"Eneo hili mliwekee alama, muandike siku na muda ambao tetemeko lilitokea," aliagiza Profesa Muhongo.
Katika
ziara hiyo, Waziri Muhongo pia amekagua miundombinu ya Shirika la
Umeme Tanzania (TANESCO) ambayo iliathiriwa na tetemeko la ardhi, ili
kubaini hatua zinazopaswa kuchukuliwa kwa lengo la kuiboresha na baadaye
leo hii atakutana na Kamati ya Maafa ili kuweka mikakati ya kusimamia
Shughuli za maafa na namna bora ya kuwaelimisha wananchi jinsi ya
kujihami kabla na baada ya Tetemeko.
EmoticonEmoticon