Moja ya Ndege mpya mbili
zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL)
ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa
sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt
Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial
Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakisubiri kuwasili kwa Moja
ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya
ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Julius leo Septemba 20, 2016
Moja ya Ndege mpya mbili
zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL)
ikipata saluti ya maji (Water Canon Salutation) toka kwa magari ya
Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mara tu bada ya kuwasili katika uwanja wa
ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akisalimiana na Rubani aliyerusha Ndege
mpya moja kati ya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni
ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt
Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial
Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakiwa kwenye Moja
ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya
ndege Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt
Leonard Chamriho akipeana mikono kwa furaha na Mkurugenzi wa Kampuni ya
Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu mara baada ya Moja
ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya
ndege Tanzania (ATCL) kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Julius leo Septemba 20, 2016, Wengine ni marubani wa ndege hiyo
PICHA NA IKULU
Ndege mpya ya kwanza iliyonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imetua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es salaam ikitokea nchini Canada ilikotengenezwa.
Ndege hiyo aina ya Bombadier
Q400 NextGen imetua majira ya saa 6:15 Mchana na kisha kupatiwa heshima
maalum ambayo hutolewa kwa ndege yoyote mpya inayotua katika nchi yake
(Water Salute).
Baada ya kupokea heshima hiyo, ndege imeegeshwa katika eneo la ndege za jeshi (Airwing Ukonga).
Akizungumza baada ya kuwasili
kwa ndege hiyo Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho amesema ndege
ya pili inatarajiwa kuwasili baada ya wiki moja na kwamba baada ya
kuwasili ndege ya pili ndipo yatafanyika mapokezi rasmi, yatakayoongozwa
na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa
tarehe itakayotangazwa baadaye
EmoticonEmoticon