ZAIDI ya Watoto 4000 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi huzaliwa kila mwaka nchini na wanaoripotiwa hospitalini si zaidi ya 500 hatua ambayo imechangia kwa asilimia kubwa ongezeko la watoto wenye mtindio wa ubongo huku baadhi yao wakipoteza maisha kwa sababu ya kukosa Tiba.
Akizungumza katika Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo wakazi wa zoezi la Upasuaji wa watoto hao
lilipokuwa likiendeshwa na madaktari Bingwa, Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya
Mifupa na Upasuaji ya (MOI)iliyopo Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili,Dkt Othman
Kiloloma alisema ongezeko la watoto hao linatokana na ukosefu wa lishe yenye
virutubisho vijulikanavyo kwa jina la “Folic Acid”
Alisema kukosekana kwa lishe hiyo
kumesababisha tatizo hilo kwa watoto ambalo lisipopatiwa ufumbuzi wa kina
linaweza kupelekea athari kubwa kwao ikiwemo vifo hali inayoweza kupunguza
jamii ambayo ingeweza kuchangia ukuaji wa uchumi katika shughuli za uzalishaji.
“Ukiangalia
kwa hivi sasa zaidi ya watoto wapato 4000 wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi
huzaliwa kila mwaka nchini na wanaoripotiwa hospitalini si zaidi ya 500 hatua
ambayo imechangia kwa asilimia kubwa ongezeko la watoto wenye mtindio wa ubongo
huku baadhi yao wakipoteza maisha kwa sababu ya kukosa hivyo jamii inapaswa
inapaswa kuwapeleka katika Hospitali ili kuweza kuchangia ukuaji wao na
maendeleo “Alisema
Akizungumzia kuhusu changamoto
zinazosababisha watoto hao kukosa huduma za upasuaji, Afisa Habari wa Taasisi
ya Afya inayojihusisha na Upasuaji wa watoto hao, Khalfani Kiwamba alisema kuwa
upungufu wa madaktari wenye taaluma ya upasuaji wa waathirika hao ni mkubwa kwa
sababu nchini wapo saba ambapo sita wapo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na
mmoja yupo hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Bugando
Kufuatia hatua hito, Viongozi wa
Taasisi za dini nchini zimeshauriwa kuwahamasisha waumini wao wenye watoto wa
aina hiyo kuwafikisha katika Hospitali kubwa za Rufaa ili waweze kushauriwa
badala ya kuwaficha watoto hao majumbani ambapo wanapofikisha miaka kumi na
kuendelea uwezekano wa kupoteza maisha ni mkubwa sana.
“Kwani hatua hiyo imechangia kwa
asilimia kubwa ongezeko la watoto wenye mtindio wa ubongo huku baadhi yao
wakipoteza maisha kwa sababu ya kukosa tiba “Alisema
Awali akizungumza katika zoezi hilo, Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Godwin
Gondwe aliipongeza taasisi inayojihusisha kusaidia sekta ya Afya na Elimu hapa
nchini (GSM) kwa kutoa matibabu ya upasuaji huo kwa watoto hali ambayo
itawasaidia kuweza kurejea kwenye hali zao za kawaida.
Alisema katika suala kama hilo jamii haina budi kuacha kuwaficha watoto
wenye matatizo hayo badala yake waona namna ya kuwasiliana na viongozi wao
ngazi za chini kuwaepusha na vifo ambavyo vinaweza kuwakumba kutokana na hali
walizonazo.
“Lakini pia lazima jamii
ibadilike kuona umuhimu wa kuacha kuwaficha watoto wenye matatizo hayo badala
yake wawapeleke kwenye hospitali zilizopo karibu nao kwa ajili ya kupatiwa
matibabu ambayo yatawasaidia kupona “Alisema.
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma kulia akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Godwin Gondwe kushoto ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni alipotembelea Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kunapofanyika zoezi la upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi lililofanywa na Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Tanga,Dkt Karia
Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(RAS) Zena Saidi akisisitiza jambo wakati Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Godwin Gondwe kushoto mwenye shuti nyeusi alipotembelea kuona zoezi la upasuaji upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi lililofanywa na Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) chini ya Ufadhili wa Taasisi ya GSM wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni,Godwin Gondwe akitoa nauli kwa mmoja kati ya wakazi wa wilaya ya Handeni ambaye alikwenda kupata matibabu ya mtoto wake mwenye kichwa kikubwa katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kwa ajili ya matibabu yanayotolewa na Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI)chini ya Ushirikiana wa Taasisi ya GMS kulia kwake ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma
upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na migongo wazi lililofanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo kwa ajili ya matibabu yanayotolewa na Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI)
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma akiteta jambo na Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(Ras)Mhandisi Zena Saidi na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Godwin Gondwe
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma akiwaonyesha Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Godwin Gondwe kulia na Katikati ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi namna mtoto aliyekuwa na kichwa kikubwa alivyofanyiwa upasuaji
Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga(Ras) Mhandisi Zena Saidi akitoa zawadi kwa mama wa mtotoambaye alifanyiwa upasuaji wa kichwa
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma akisisitiza jambo kwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma akimuangalia mtoto aliyefanyiwa upasuaji wa kichwa kikubwa
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani Kiloloma aksisitiza jambo kwa viongozi hao kuhusiana na huduma hizo
Kaimu
Mkurugenzi wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika
Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam Dkt Othumani
Kiloloma akizungumza na waandishi wa habari |
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Taasisi ya GSM mara baada ya kufanyika zoezi la upasuaji kwa watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi lililofanywa na Taasisi ya Mifupa na Upasuaji (MOI) iliyopo katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar Es Salaam. |
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Godwin Gondwe ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Handeni akitazama jambo mara baada ya kumalizika zoezi la upasuaji huo |
EmoticonEmoticon