Mchezaji Asad Ali Juma wa timu ya
Taifa ya vijana Serengeti Boys akikokota mpira mbele ya wachezaji wa
timu ya Vijana ya Afrika Kusini katika mchezo wa kufuzu katika fainali
za Mataifa ya Afrika zitakayofanyika nchini Madagascar uliofanyika
kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi wilaya ya Temeke jijini Dar es
salaam.
Katika kipindi cha pili mchezaji
Ibrahim Abdallah ameifungia goli la pili timu ya Serengeti Boys ,
Wakati kipindi cha kwanza mchezaji wa Serengeti Boys Rashid Abdalla
alifunga goli la kwanza.
Kwa matokeo hayo Serengeti Boys
inasonga mbele katika michuano hiyo ya vijana baada ya kuitoa timu ya
Afrika Kusini kwa magoli 3-1 kufuatia sare ya magoli 1-1 nchini Afrika
Kusini, Ambapo inatarajiwa kukutana na timu kati ya Namibia au Congo
Brazaville.
Mchezaji Ibrahim Abdallah kushoto
akisahangilia na wenzake mara baada ya kuifungia goli la pili timu ya
Serengeti Boys kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi
Waziri wa Habari , Utamaduni ,
Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akizungumza kwa furaha mara baada ya
timu ya Serengeti Boys kuifunga timu ya Afrika Kusini kwenye uwanja wa
Azam Chamazi magoli 3-1
Vikosi vya timu hizo vikiingia uwanjani kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Kikosi cha timu ya vijana ya Afrika Kusini
Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Serengeti Boys kikiwa katika picha ya pamoja.
Viongozi wa shirikisho la mpira wa
miguu Tanzania wakiwa katika jukwaa kuu kulia ni Celestin Mwesigwa
nakushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira Tanzania Jamal Malinzi pamoja
na viongozi wengine.
Benchi la Ufundi la Serengeti Boys.
Benchi la Ufundi la timu ya taifa ya Afrika Kusini.
EmoticonEmoticon