PROF. MBARAWA ASISITIZA TATHIMINI UWANJA WA NDEGE SONGWE

August 04, 2016


br1 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipata maelezo ya mfumo wa utabiri wa hali ya hewa katika Uwanja wa Kimataifa wa Songwe (SIA) kutoka kwa Mtaalam wa masuala ya hali ya hewa uwanjani hapo, Wakati alipokagua uwanja huo mkoani Mbeya.
br2 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akipata maelezo kutoka kwa Bw. Baraka Mwambipile kuhusu namna ndege zinavyoongozwa wakati wa kuruka na kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Songwe, Wakati alipokagua uwanja huo mkoani Mbeya.
br3 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata ufafanuzi wa michoro ya ujenzi wa jengo la abiria kutoka kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) wakati alipokagua Uwanja wa Ndege wa Songwe, Mkoani Mbeya.
br4 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo  kwa Mhandisi wa Mamlaka ya Viwanja vya ndege (TAA) kuhusu ujenzi wa jengo la pili la abiria katika Uwanja wa Ndege wa Songwe, wakati alipokagua uwanja huo Mkoani Mbeya.
br5 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia) akiendelea na ukaguzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Songwe, Mkoani Mbeya.
br6 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na ukaguzi wa wa Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Songwe , Mkoani Mbeya.
br7 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia) akitoa maelekezo  kwa Mkandarasi wa kampuni ya Shapriya Co Ltd anayejenga jengo la pili la abiria wakati alipokagua uwanja wa kimataifa wa Songwe, Mkoani Mbeya.
………………………………………………………………………………………………….
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa Serikali haitaendelea na ujenzi wa jengo la pili la abiria katika uwanja wa ndege wa Songwe uliopo mkoani Mbeya mpaka tume ya watalamu iliyoundwa kuchunguza ili kujiridhisha kama utaratibu ulizingatiwa kabla ya kuaza ujenzi huo.
Prof. Mbarawa ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua jengo hilo linalojengwa na mkandarasi wa Kampuni ya Db Shapriya ya Tanzania ambapo amesema hadhi ya jengo hilo hairidhishi hivyo ipo haja ya kujiridhisha kama taratibu zote zilifuatwa kabla ya ujenzi.
Amebainisha kazi ya tume hiyo ya wataalamu ni kuhakiki namna utaratibu wa kumpata mkandarasi ulivyofanywa, gharama halisi za mradi na fedha iliyolipwa kwa mkandarasi kama inaendana na thamani ya jengo hilo.
“Serikali haiwezi kutoa fedha ya kumalizia jengo hili kabla ya kujiridhisha ili kuhakikisha fedha tutakazozitoa zitatumika kulingana na ilivyopangwa na thamani ya fedha inaendana na jengo lenyewe”, amesema Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha Waziri Prof. Mbarawa ameeleza  ili kuwa na miundombinu imara na ya kudumu ni lazima kuhakikisha miradi ya ujenzi wa miundombinu inasimamiwa vizuri na taratibu   za kupata mkandarasi bora zinafuatwa.
“Kutokuwa na miundombinu isiyo imara ni sababu ya wahusika kuweka mbele maslahi binafsi na siyo ya Taifa”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa
Pia ameutaka uongozi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kuhakikisha makosa yaliyojitokezo kwenye ujenzi wa jengo la abiria katika uwanja wa ndege wa Mwanza hayajirudii katika kiwanja hiki.
Kwa upande wake Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Songwe Bw. Hamisi Amiri amemhakikishia Waziri Mbarawa kusimamia ujenzi uliobaki kwa kuzingatia taratibu na makubaliano yaliyowekwa ili jengo hilo lidumu kwa manufaa ya Taifa na Mkoa.
Uwanja wa Songwe ni kiungo muhimu kwa wananchi wa mikoa ya Katavi, Rukwa, Njombe na Ruvuma na katika mwaka huu wa fedha umetengewa kiasi cha shilingi bilioni 10 kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa jengo la abiria na taa uwanjani hapo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »