Meneja Chapa wa Kampuni ya Simu ya Tigo, William Mpinga (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Kampuni hiyo, Kijitonyama Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu kampuni hiyo kuanzisha kifurushi kipya mahsusi cha miito na data katika tamasha la Fiesta 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa Tamasha la Fiesta, Sebastian Maganga.
Mwenyekiti wa Tamasha la Fiesta, Sebastian Maganga (kushoto), akizungumzia kukamilika kwa maandalizi ya tamasha hilo.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya simu ya Tigo imetangaza vifurushi viwili vipya vya miito na data vinavyofahamika kama ‘Vifurushi vya Fiesta’ (Fiesta packages) ambavyo vinalenga kuwanufaisha watega wote wa Tigo na wasio wakati wa tamasha la Fiesta 2016.
Vifurushi hivi vya kuvutia vitakuwa vinapatikana kwa wateja wote watakaohudhuria matamasha na hata wasio hudhuria.
Vifurushi vipya vitawawezesha wateja kuchagua kati ya data za GB 1 au visivyo na ukomo ambavyo vinajumuisha dakika 490 Tigo kwenda Tigo, dakika 10 mitandao yote na SMS 100 kwa shilingi 1000 wakati wale ambao sio wateja wa Tigo ambao wamenunua kadi ya simu ya 4G ya Tigo watapata dakika 60, sms 60 na MB 60 papo hapo pindi wanapojisajili na baadaye kuchagua kati ya data na kifurushi kisicho na ukomo.
Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari katika makao makuu ya Tigo, Meneja Chapa, William Mpinga alisema, “vifurushi hivi vimekuwa ikiwa ni ahadi tulioyoitoa kwa wateja wetu kuhusu ofa mbalimbali na promosheni ambazo zitakuwepo wakati wa msimu wa Fiesta 2016. Hali kadhalika tutaendelea na uanzishaji wa bidhaa na huduma za ubinifu ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu na pia kutoa nafasi kwa wateja wapya.”
Mpinga alifafanua kuwa tamasha la Fiesta 2016 linawakaribisha Watanzania wote na kuongeza kuwa pia tukio hilo litatoa shughuli zenye mabadiliko kijamii.
Mpinga alisema, “Mwanzoni wa wiki iliyopita tulianzisha kauli mbiu ya tamasha la fiesta inayosema, "Fiesta 2016 Kwa Kishindo cha Tigo, Imooooo!" ambapo mantiki iliyopo katika kauli mbiu hii ni kutoa bidhaa na huduma ambazo ni mahsusi kwa wateja wetu katika kipindi cha tamasha.”
Mwenyekiti wa Tamasha la Fiesta 2016, Sebastian Maganga alisema, “ Tunafurahi sana kutangaza kwamba tamasha la Fiesta 2016 litaanza rasmi jijini Mwanza Agosti 20, 2016. Kwa hiyo wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake watarajie kupata vifurushi hivi maalum pamoja na shughuli za kufurahisha katika kipindi cha wiki nzima kabla ya tamasha.”
Tamasha la Fiesta 2016 linaandaliwa kila mwaka na kampuni ya Prime Time Promotions, na hivi sasa ni mwaka wa 15 tangu kuanziswhwa kwake na linatarajiwa kujumuisha mikoa 15 ambayo ni pamoja na Mwanza, Kahama, Kagera, Musoma, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro, Tanga, Kilimanjaro, Mtwara, Iringa, Mbeya na Dar es Salaam.
Tamasha la Fiesta 2016 linafanyika kwa ushirikiano wa Prime Time Promotions na Tigo Tanzania ambayo ni mdhamini mkuu.
EmoticonEmoticon