Waziri
wa Nchi Ofisi ya Raid TAMISEMI George Simbachawene akikagua jengo la
darasa la while ya msingi Luegu wilaya ya Namtumbo baada ya kupata maafa
mwaka uliopita.Waziri ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Namtumbo kutoa fedha shilingi milioni 10 kwa ajili ya Ujenzi
wa vyoo vya kudumu vya wanafunzi ndani ya mwezi mmoja.
Wanafunzi
wa kidato cha Tano shule ya sekondari Nasuli wilaya ya Namtumbo
wakimsikiliza Waziri Simbachawene alipotembelea shule ambayo imeanzisha
madarasa ya kidato cha tano mwaka huu.Jumla ya wanafunzi 90 wasichana
wameanza masomo hadi sasa.
Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Dkt.Binilith Mahenge akimpongeza Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais,TAMISEMI George Simbachawene alipomaliza kukagua ujenzi wa
barabara ya lami ya FFU-Matogoro yenye urefu wa kilometa 3.2 kwenye
Manispaa ya Songea.
Jengo
la makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Songea lililokamilika
kujengwa ambalo leo limekaguliwa na Waziri Simbachawene kwenye kijiji
cha Lundusi,Peramiho.Waziri Simbachawene ameagiza ifikiapo tarehe 05
Agosti 2016 watumishi wote wa Halmashauri ya wilaya ya Songea wahamie na
kuendelea na kazi baada ya kukamilika ujenzi wake.
Wananchi
wa kijiji cha Lundusi Peramiho wakiwa kwenye mkutano wa hadhara
uliohutubiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI George
Simbachawene(hayupo pichani) wakati wa ziara yake Mkoani Ruvuma leo
EmoticonEmoticon