Gondwe alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wafanyabiashara, viongozi wa dini ambapo pamoja na mambo mengine aliwataka kuona umuhimu wa kutumia fursa ya uwepo wa rutuba nzuri ya ardhi iliyopo wilayani humo kujikita kulima kisasa ili kuweza kupata mafanikio.
Alisema kuwa lazima wafanyabiashara watambue kuwa kilimo ndio njia pekee ambayo inaweza kuwainua kiuchumi na kuharakisha kasi ya ukuaji wa maendeleo iwapo watazingati na kukipa kipaumbele kila wakati
“Niwaombeni suala la kilimo mlipe msukumo mkubwa sana kwani hii ndio njia pekee ambayo inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kusukuma gurudumu la maendeleo kwa wilaya yetu “Alisema.
Aidha pia alisisitiza umuhimu wa wananchi wa wilaya hiyo kutilia mkazo kulima mazao yanayostahimili ukame ikiwemo Alizeti, Ufuta,Viazi na Mihogo ili kuweza kukabiliana na tatizo la kutoku patikana mvua za uhakika kwa ajili ya kilimo cha mahindi.
“ Ninajua katika kipindi hiki tumelima kwa wingi lakini hali ya hewa sio nzuri na mvua nazo zimekuwa hazipatikana kwa uhakika hivyo lazima wakulima tubadilike kwa kuanza kupanda mazao yanayostahimili ukame ili kuweza kuepukana na baa la njaa “Alisema DC Gondwe.
Sambamba na hayo,Mkuu huyo wa wilaya alizishauri taasisi za kibenki wilayani humo kuhakikisha zinatoa kipaumbele kwa wawekezaji wa kilimo ili waweze kuzalisha kwa wingi mazao ambayo yataweze kuinua kiuchumi lakini pia kuchangia pato la Taifa.
Hata hivyo ,Mkuu huyo wa wilaya alitumia pia fursa hiyo kuwaasa wakulima waliopata mazao kidogo kuhakikisha wanayatunza na kuacha kuyauza kwani kufanya hivyo kutaweza kusababisha hali ya njaa kwao
Naye Sherhe wa wilaya ya Handeni, Shabani Mohamed alisema kuwa wao watamuombea dua Mkuu huyo wa wilaya ili mungu amuwezeshe kuweza kutimiza majukumu yake ipasavyo na kusaidia kuchangia juhudi za maendeleo kwa wananchi.
“Nikuambie Mh Mkuu wa wilaya ujio wako hapa Handeni watu wengi wamefurahi sana kwani uchapakazi wako unafahamika tokea ulipokuwa unafanya kazi kwenye kituo cha ITV na tunaamini uhodari huo pia utasaidia kuinua uchumi wetu “Alisema.
Alisema kuwa wao watahakisha wanampa ushirikiano wa hali ya juu ili kumuwezesha kutekeleza vema majukumu yake ya kuipa maendeleo wilaya hiyo.
EmoticonEmoticon