Waziri
Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais Mstaafu Mzee John Samwel Malecela
amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana kufufua zao la
Zabibu Mkoani humo kwa kuzishughulikia changamoto zinazodidimiza kilimo
cha zao hilo.
Mzee
Malecela pia amemtaka Mheshimiwa Rugimbana kutekeleza agizo la
Mheshimiwa Rais Magufuli la kuondoa Tatizo la njaa Mkoani Dodoma kwa
kuzifuatilia skimu zote za kilimo zinazolegalega na zile zilizokosa
uongozi imara.
Aliyasema
hayo mwishoni mwa wiki walipoambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.
Jordan Rugimbana kwenye ziara ya kukagua skimu ya umwagiliaji ya zabibu
ya Chinangali II yenye jumla ya ekari 1,250 iliyopo Chamwino ambayo kwa
sasa inalegalega na kumtaka Mkuu wa Mkoa kuingilia kati kunusuru skimu
hiyo inayokabiliwa na changamoto za kukosa uongozi imara na uendeshaji
wa kilimo usio zingatia kanuni za kilimo bora.
Aliitaka
serikali kusaidia wakulima wa chama cha CHABUMA wanaomiliki skimu hiyo
ya zabibu ya Chinangali ili waweze kuanzisha kiwanda cha kusindika
mchuzi wa zabibu na kusema kuwa kufanya hivyo kutawaepusha wakulima wa
zabibu dhidi ya wafanyabiashara walanguzi wanaowalalia wakulima wakati
wa mavuno ya zabibu.
Katika
hatua nyingine, Mzee Malecela amemtaka Mheshimiwa Rugimbana kuondoa
tatizo la njaa kwenye Mkoa wa Dodoma kwa kufufua skimu zote zilizokufa
na zile zinazolegalega Mkoani hapa ili ziweze kuzalisha chakula na
ametaka mkazo mkubwa uwekwe kwenye kilimo cha umwagiliaji kwa kuwa Mkoa
wa Dodoma una maji mengi chini ya ardhi.
Amesema
serikali inaingia gharama kubwa sana kuanzisha skimu za umwagiliaji
lakini nyingi zinakosa ufuatiliaji na uongozi imara matokeo yake
zinakufa akitolea mfano skimu ya Mgangalenga iliyopo Mpwayungu Chamwino
yenye zaidi ya Ekari 20,000. Kwa mujibu wa Katibu Tawala msaidizi wa
Uchumi na Uzalishaji Bi. Aziza Mumba amesema Mkoa wa Dodoma una skimu za
umwagiliaji zipatazo mia tatu (300).
Mkuu
wa Mkoa Mheshimiwa Rugimbana amekubali ushauri huo na kuahidi kuufanyia
kazi kwakuwa agizo la kuondoa njaa ni moja ya maagizo aliyopewa na
Mheshimiwa Rais Magufuli. Amesema kwanza atakua mlezi wa skimu ya zabibu
ya Chinangali, na kuwa atafanya jitihada za kutafuta wafadhili kwa
lengo la kuwezesha mradi wa kiwanda cha kusindika mchuzi wa zabibu.
Pamoja
na kutembelea skimu hiyo ya Chinangali, Mkuu wa Mkoa ameahidi
atazitembelea skimu zote mia tatu (300) ili kubaini changamoto za kila
skimu na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi ili zote ziweze kuzalisha kisasa
na kusaidia katika jitihada za kuondoa tatizo la njaa.
Rugimbana
amesema tayari ameshaunda kikosi kazi kwa ajili ya kushughulikia
masuala ya uzalishaji katika miradi ya Kilimo na Mifugo na moja kati ya
jukumu kubwa alilokipa kikosi kazi hiko ni kubaini changamoto za skimu
hizi za umwagiliaji, kuhakikisha kinakua nazo karibu na kuzijengea uwezo
ikiwa ni pamoja na kuimarisha uongozi wa skimu hizo zote na uzalishaji
kwa ujumla.
Waziri
Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela
akiwa ameongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana
wakisalimiana na Viongozi wa skimu ya Umwagiliaji ya zabibu iliyopo
Chinangali II Chamwino wakati walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa
wiki.
Afisa
Kilimo Wilaya ya Chamwino Ndg. Godfrey Mnyamale akiwasilisha taarifa ya
mradi wa skimu ya Umwagiliaji wa zabibu ya Chinangali II kwa mkuu wa
Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana na Mzee Malecela (hawapo pichani) wakati
walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki. Wengine ni viongozi wa
skimu hiyo.
Waziri
Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela
akimweleza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana (kushoto) changamoto
zinazo didimiza kilimo cha Zabibu Dodoma na kumtaka kufanya kila awezalo
kufufua zao hilo sambamba na kuondoa tatizo la njaa Dodoma wakati
viongozi hao walipotembelea skimu ya Umwagiliaji wa zabibu ya Chinangali
II mwishoni mwa wiki.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana akiahidi kufufua zao la zabibu
Mkoani humo na kuondoa tatizo la njaa kwa kufufua skimu zote za
umwagiliaji zinazolegalega na kukosa uongozi imara wakati akizungumza
na viongozi wa skimu ya umwagiliaji wa Zao la zabibu iliyopo Chinangali
II Chamwino mwishoni mwa wiki.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana na Waziri Mkuu na Makamu wa
kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela wakikagua mitambo ya
kusukuma maji kwenye skimu ya Umwagiliaji ya zabibu iliyopo Chinangali
II Chamwino wakati viongozi hao walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa
wiki, wengine ni viongozi wa skimu hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana na Waziri Mkuu na Makamu wa
kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela wakikagua miundombinu
ya maji kwenye skimu ya Umwagiliaji ya zabibu iliyopo Chinangali II
Chamwino wakati viongozi hao walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa
wiki, wengine ni viongozi wa skimu hiyo.
Waziri
Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela
na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana wakikagua shamba la zabibu la
Chinangali II Chamwino linalotumia teknolojia ya Umwagiliaji wa matone
wakati viongozi hao walipotembelea skimu hiyo mwishoni mwa wiki, wengine
ni viongozi wa skimu hiyo.
Waziri
Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais mstaafu Mzee John Samwel Malecela
akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jodan Rugimbana jinsi tatizo la
fangasi linavyoshambulia zao la zabibu wakati wakikagua shamba la zabibu
la Chinangali II Chamwino wakati viongozi hao walipotembelea skimu hiyo
mwishoni mwa wiki, wengine ni viongozi wa skimu hiyo.
Sehemu
ya Skimu ya zabibu ya Chinangali II iliyopo Chamwino inayotumia
teknolojia ya umwagiliaji wa matone, kwa sasa skimu hiyo na nyingine
baadhi Mkoani humu zinalegalega kutokana na kukabiliwa na Changamoto
kadhaa wa kadhaa ambazo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana
ameahidi kuzitafutia ufumbuzi.
Sehemu
ya kitalu cha kuzalisha miche kwenye Skimu ya zabibu ya Chinangali II
iliyopo Chamwino, kwa sasa skimu hiyo na nyingine baadhi Mkoani humu
zinalegalega kutokana na kukabiliwa na Changamoto kadhaa wa kadhaa
ambazo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Jordan Rugimbana ameahidi kuzitafutia
ufumbuzi.
EmoticonEmoticon