Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amempokea
Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda kwa ziara rasmi ya
kiserikali. Rais Magufuli ameambatana na Mkewe Mama Janeth Magufuli na
Rais Kagame ameambatana na mkewe Mama Jeannette Kagame. Ziara hii ni ya
siku mbili.Baada ya Hapo ataelekea Ikulu jijini Dar es Salaam kwaajili
ya Kufanya Mazungumzo.Baada ya hapo wataelekea katika Viwanja vya
Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam kwa ajili ya
ufunguzi rasmi wa maonesho hayo ya 40 ya Kimataifa katika viwanja vya
Sabasaba ,jijini Dar.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aakiwa
ameambatana na mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda
mara baada ya kuwasili asubuhi hii katika uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere kwa ziara rasmi ya siku mbili ya kiserikali. Rais
Magufuli ameambatana na Mkewe Mama Janeth Magufuli na Rais Kagame
ameambatana na mkewe Mama Jeannette Kagame.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na
mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda wakipata Gwaride
la heshima uwanjani hapo.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na
mgeni wake Mhe. Paul Kagame Rais wa Jamhuri ya Rwanda wakitazama kikundi
cha ngoma za asili kilichokuwa kikitumbuiza uwanjani hapo.
Rais
Paul Kagame akiwapungi mkono baadhi ya wananchi mbalimbali waliofika
kumlaki uwanjani hapo,kushoto kwake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli .