Kampuni ya Bia Serengeti yazindua mradi wa maji wa 81m/- Katesh, Hanang

June 24, 2016

Mradi wa maji  wenye thamani ya shilingi milioni 81 mjini Katesh wilayani Hanang uliofadhiliwa na kampuni ya bia ya serengeti ikiwa ni mkakati wa kuwapatia wakazi wa eneo hilo maji safi na salama.

Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti John Wanyancha akizungumza na wananchi wa katesh wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji wenye uwezo wa kuhudumia wakazi wapatao 12000 katika hafla iliyofanyika siku ya jumanne june 22 wilayani Hanang ,mkoa wa Manyara.


Diwani wa Kata ya Gidahababieg,Hassan Hilbagiroy akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kata hiyo mara baada ya uzinduzi wa mradi wa maji uliofadhiliwa na kampuni ya bia ya serengeti katika hafla iliyofanyika siku ya jumanne june 22 wilayani Hanang, mkoa wa Manyara.

Mmoja wa wakazi wa Kata ya Gidahababieg,Katesh akifurahia maji mara baada ya ufunguzi wa mradi wa maji uliofadhiliwa na kampuni ya bia ya serengeti katika hafla iliyofanyika siku ya jumanne june 22 wilayani Hanang, mkoa wa Manyara.


Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Thobias Mwilapwa akiwa na picha ya pamoja na wananchi mara ya baada ya ufunguzi wa mradi wa maji uliofadhiliwa na kampuni ya bia ya serengeti katika hafla iliyofanyika siku ya jumanne june 22 wilayani Hanang mkoa wa Manyara.



Hanang, Juni 22, 2016- Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) leo imezindua mradi wa maji  wenye thamani ya shilingi milioni 81 mjini Katesh wilayani Hanang’ ikiwa ni mkakati wa kuwapatia wakazi wa eneo hilo maji safi na salama.

Mradi huo wenye uwezo wa kuwahudumia watu 12,000 unajumuisha kisima kilichochimbwa pamoja na mifumo yake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua na tenki la maji ukiwa na uwezo wa kuzalisha  lita 45,000 za maji kila baada ya saa sita.

Akizungumza latika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni ya Bia ya Serengeti John Wanyancha,  alisema kuwa kisima hicho ni mkakati wa kampuni hiyo ya bia wa kuisaidia jamii chini ya mpango uitwao Maji ya Maisha na kuongeza kuwa SBL imeshatekeleza  miradi kama hiyo katika mikoa ya   Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma  ambayo imenufaisha watu zaidi ya milioni moja kwa kuwapatia maji safi na salama.

Wanyancha alisema kuwa mradi wa Katesh  sio tu kwamba utaboresha afya za wenyeji wa eneo husika bali pia utaongeza uzalishaji  kiuchumi “hususani miongoni mwa wanawake na watoto wa kike  ambao hawatalazimika kutumia saa nyingi   kutafuta maji sehemu nyingine. Hii inatoa fursa kwa watoto wa kike kuhudhuria masomo shuleni.”

“Kampuni ya Bia ya Serengeti ina sera iliyojikita katika kuleta ustawi wa jamii ambapo Maji ya Uhai ni mojawapo ya maeneo manne iliyoyapa kipaumbele. Maeneo mengine utoaji wa Stadi za Maisha, Uendelevu wa Mazingira na Kuhimiza Unywaji wa pombe Kistaarabu.

Mkurugenzi huyo wa mahusiano aliongeza kuwa SBL  ina programu ya kilimo  ambayo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita imewasaidia  wakulima zaidi ya 100  hapa nchini kwa kuwapatia misaada ya kitaalamu na kifedha ambapo imewasaidia  kuboresha maisha yao pamoja na maisha ya jamii zao.

Aidha Wanyancha aliongeza: “Kupitia mpango huu wa kusaidia SBL imeweza kuongeza upatikanaji wa shayiri inayotumika kama malighafi katika utengenezaji wa bia kutoka tani sifuri 10,000 jambo ambalo limechochea ukuaji wa kasi wa kampuni yetu.”

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Tobias Mwilapwa  ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ameipongeza kampuni ya SBL kwa kuwa mstari wa mbele katika kusaidi miradi ya kijamii nchini jambo ambalo amesema ni chachu katika kuiletea jamii maendeleo.

“Licha ya  kuchangia katika  kukua kwa uchumi wa taifa  kupitia malipo ya kodi kwa wakati, kampuni ya Serengeti  imetoa mchango muhimu katika maendeleo ya taifa  hususani katika uzinduzi wa huduma za miradi ya maji safi na salama  nchini,” alisema.

photo Krantz Mwantepele Founder & CEO , KONCEPT Phone: +255-712579102 /+255-767392840 Email: krantzcharles@gmail.com Blog: www.mwanaharakatimzalendo.blogspot.com Website;www.koncept.co.tz

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »