Meneja
Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, katikati
akizungumza baada ya kumpa hati yake mteja wao wa viwanja vya Vikuruti,
wilayani Kibaha, mkoani Pwani, Ibrahim D Mahinya. Kulia ni Afisa Sheria
wa Bayport, Mrisho Mohamed.
TAASISI ya
Kifedha ya Bayport inayojihusisha na mikopo imeendelea kugawa hati za viwanja
kwa wateja wao walionunua viwanja katika mradi wao uliopo Vikuruti, wilayani
Kibaha, mkoani Pwani, uliozinduliwa rasmi mwezi Mei mwaka jana.
Wateja waliokabidhiwa hati zao ni pamoja
na Ibrahim D Mahinya na Desdery Selestine Mkenda ambao wote kwa pamoja walikuwa
miongoni mwa wateja waliojiunga na huduma hiyo ya mikopo ya viwanja vya
Bayport.
Ibrahim
Mahinya kushoto akizungumza jambo baada ya kukabidhiwa hati ya kiwanja
cha Vikuruti, kutoka Bayport Financial Services, jijini Dar es Salaam
leo asubuhi. Mwenye miwani ni Meneja Biashara wa Bayport Financial
Services, Thabit Mndeme na Mrisho Mohamed, Afisa Sheria wa Taasisi hiyo
inayohusisha na mikopo ya fedha na bidhaa vikiwamo viwanja.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam katika makabidhiano hayo, Meneja Biashara wa
Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema kusudio lao ni kugawa
hati kwa wateja wao mapema iwezekanavyo ili kujitofautisha na wadau
wengine wanaojihusisha na mambo ya uuzaji wa ardhi kwa njia mbalimbali.
Meneja
Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme katikati
akimkabidhi hati ya kiwanja cha Vikuruti mteja wao Desdery Selestine
Mkenda. Kulia ni Mrisho Mohamed, Afisa Sheria wa Taasisi hiyo
inayohusisha na mikopo ya fedha na bidhaa vikiwamo viwanja.
Alisema
kwamba hati zinazotoka kwa mwaka huu ni zile zinazohusu wateja
walionunua viwanja hivyo katika mradi wa Vikuruti, Mlandizi, wilayani
Kibaha, mkoani Pwani, mradi uliopokewa vizuri na Watanzania, jambo
lililochangia Bayport kupanua wigo huo kwa kuanzisha miradi mingine ya
Bagamoyo, Kigamboni, Chalinze, Kibaha na Kilwa.
Meneja
Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, akimkabidhi hati
ya kiwanja cha Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani Ibrahim D
Mahinya. Picha na Mpiga Picha Wetu.
Mteja wa kiwanja cha Vikuruti vinavyotolewa na Bayport, Ibrahim D Mahinya akizungumza jambo.
Ibrahim Mahinya, akitia sahihi ya dole gumba kama njia ya kukamilisha utaratibu wa makabidhiano ya hati yake.
Thabit Mndeme katikati akizungumza kwenye makabidhiano hayo ya hati za viwanja.
Mteja
wa viwanja vya Vikuruti, Desdery Mkenda kushoto akishuhudia nyaraka
zinazohusiana na mambo ya hati yake aliyokabidhiwa baada ya kuwa
miongoni mwa Watanzania waliojitokeza kununua viwanja vya Bayport
vilivyopo Vikuruti, wilayani Kibaha, mkoani Pwani. Katikati ni Meneja
Biashara wa Bayport, Thabit Mndeme na Afisa Sheria wa taasisi hiyo
Mrisho Mohamed.
Meneja
Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, kulia akipeana
mkono wa na mteja wao Ibrahim Mahinya baada ya makabidhiano ya hati yake
ya kiwanja cha Vikuruti kukamilika.
“Tumepania
kuwa tofauti na wadau wengine wanaotoa huduma ya ardhi, kwa kuhakikisha mteja
wetu anapata hati yake haraka na bila usumbufu wowote kwa ajili ya kumuondolea
kero za ufuatiliaji wa hati.
“Tunawaomba
Watanzania waendelee kuiunga mkono Bayport kwa kuchangamkia fursa za mikopo
katika miradi yetu yote ukiwamo wa Chalinze, Kigamboni, Kilwa, Kibaha na
Bagamoyo ambayo vinauzwa kwa mita moja ya mraba Sh 10,000 Bagamoyo, Chalinze Sh
4500, Kibaha Sh 9000, Kilwa Sh 2000 na Kigamboni Sh 10000,” Alisema Mndeme.
Naye Mahinya
aliyekabidhiwa hati yake kutoka Bayport alisema kwamba amefurahishwa kupewa
hati kwa haraka jambo ambalo ni tofauti na matarajio yake kutokana na suala
hilo kuwa na mzunguuko mkubwa.
“Nimepata
hati yangu kwa haraka mno, hii ni tofauti na matarajio yangu kwa sababu
nafahamu suala la hati linavyokuwa na mkanganyiko mkubwa kwa sababu
linashirikisha mikono ya watu wengi na lina mambo mengi pia, ila kwa Bayport
kila kitu kinakwenda vizuri, hivyo nalazimika kusema kuwa utaratibu wa kazi wa
taasisi hii umenivutia,” Alisema.
Mteja
mwingine Mkenda aliwashukuru Bayport kwa kumpatia hati yake, baada ya kuwa
mmoja wa Watanzania aliyejipatia viwanja vya Vikuruti vilivyozinduliwa na
taasisi hiyo mwaka jana mwezi wa tano, huku huduma hiyo ya viwanja ikipatikana
katika ofisi zote za Bayport.
EmoticonEmoticon