Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa Tanga, Jabir Bundile akiwa kwenye banda lao lililopo kwenye maonyesho hayo
Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa
Tanga, Jabir Bundile wa pili kulia akitoa elimu kwa mkazi wa Tanga namyanatolewa na mfuko huo.
na ya mafao WAKAZI wa Mkoa wa Tanga wametakiwa kutumia fursa ya kujiunga na Mfumo
wa wote scheme unaotolewa na Mfuko wa Pensheni PPF ili kuwawezesha
kukithi mahitaji kwa sababu unalengo kuu la kutambua mchango wa
ushiriki kwenye sekta isiyo rasmi katika kuinua uchumi.
Hayo yalisemwa jana na Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF Mkoa wa
Tanga, Jabir Bundile wakati alipozungumza na gazeti hili katika
maonyesho ya nne ya biashara ya kimataifa ya Tanga yanayofanyika
kwenye viwanja vya Mwakidila jijini hapa ambapo alisema mfumo huo
utasaidia kufikia wananchi wengi.
Alisema kuwa fao hilo likuwa likitoa fursa mbalimbali kwa wafanyakazi
waliopo kwenye sekta iliyo rasmi na isiyorasmi ili kuwawezesha
kunufaika na mfumo huo kwa ajili ya kukuza shughuli mbalimbali za
kiuchumi na kijamii kwa mustakabali wa maendeleo yao.
“Niwaambieni kila mtu au kikundi chenye mlengo wa kiuchumi kilichopo
kwenye sekta isiyorasmi kama vile wakulima, wafugaji, wavuvi, mama
lishe, waendesha pikipiki, wajasiriamali wadogo wadogo kwa lengo la
kuhakikisha wananufaika kupitia mfumo huo “Alisema.
Aliongeza kuwa pia mfumo huo unawagusa wasanii, wana michezo,
wachimbaji madini wadogo wadogo wanaweza kujiunga na mfumo huo kwa
lengo la kupata manufaa yanayotokana na mfuko huo.
Sambamba na hilo pia alisisitiza uwepo wa mafao yanayotolewa na mfuko
huo kuwa ni ule wa Afya, Fao la Uzeeni, Mkopo wa elimu ambao unalengo
la wanachama kukopa na kujiendeleza kielimu na PPF na mkopo ambao
unakuwezesha kutimiza ndoto yako.
EmoticonEmoticon