Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano
na Mazingira Mh.Luhaga Mpina wa kwanza kushoto,katikati aliyevaa kanzu
ni mbunge wa Temeke(CUF)Mh.Abdallah Mtolea wakitembezwa sehemu mbalimbali
za kiwandani hapo mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa raisi Muungano
na Mazingira Mh.Luhaga Mpina akipata maelezo jinsi gani kiwanda hicho
kinavyochuja maji kwa njia ya kisasa kabisa kwaajiri ya matumizi na
uzalishaji kiwandani hapo.
Kiwanda cha bia aina ya serengeti kilichopo chang'ombe wilaya
ya Temeke jijini Dar es salaam kimepigwa faini ya shillingi za kitanzania
millioni kumi na sita(16)na Baraza la usimamizi wa mazingira Nchini(NEMC)baada
ya kutokutimiza masharti ya sheria ya mazingira ya mwaka(2004)na kanuni
zake.
Uamuzi huo umefikiwa baada ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa raisi Muungano na mazingira Mh.Luhaga Mpina kupata malalamiko
kutoka kwa wanainchi wanaozunguka maeneo ya kiwanda hicho na kuainisha
uchafuzi wa mazingira yanayowazunguka wananchi hao na kuhatarisha
usalama wa afya zao,ambapo ilimlazimu naibu waziri kufanya ziara ya
kushtukiza kiwandani hapo,huku akiambatana na Wakurugenzi kutoka Baraza
la usimamizi wa mazingira nchini(NEMC)na kujionea uharibifu huo.
Mh.Mpina ameagiza kiwanda hicho kulipa faini hiyo na kurekebisha
miundo mbinu hiyo ndani ya siku arobaini na tano kusiwepo tena na utiririshaji
maji machafu na yenye kemikali kali za sumu ambayo yanatoa harufu mbaya
inayohatarisha afya za wakazi wa chang'ombe wilaya ya temeke.
Pia mkurugenzi wa mazingira Bw. Boniventure Baya ametoa siku saba
kwa kiwanda hicho kiwe kimelipa faini hiyo vinginevyo hatua kali za
kisheria zitachukuliwa kutokana na kwamba wamekua wakikaidi maagizo
yanayotolewa na Baraza hilo la mazingira nchini(NEMC)na kuwataka kufanya
hivyo haraka iwezekanavyo baada ya kukiuka sheria ya utunzaji mazingira
ya mwaka(2004) na kutokutimiza masharti waliyopewa takribani miaka miwili
iliyopita.
Naye mbunge wa Temeke(CUF) Mh.Abdallah Mtolea alisema kiwanda hicho
kimekua na mahusiano mabaya na wananchi wanaozunguka maeneo jirani
na kiwanda hicho hivyo kupelekea kuwa na mgogoro wa muda mrefu na uongozi
kiwandani hapo na kumuomba Naibu waziri kutatua tatizo hilo ambalo
limekua likifanywa kwa makusudi na na uongozi wa kiwanda hicho ilihali
wanajua madhara ya wanayoyapata wananchi.
Aidha kwa upande wake afisa mazingira wa kiwanda hicho Bw.Simon Peter
alipinga vikali tuhuma hizo ambazo zimeelekezwa katika kiwanda hicho
na kusema uongozi wa kiwanda hicho unafanya kila jitihada ili kuweza
kutatua kero hiyo na si kweli kwamba hawashughulikii tatizo hilo la
mazingira jirani na wakazi hao.
Kwa upande wao wananchi kupitia kwa Bi.Emanuela Peter,walisema hiyo
ni kero kubwa sana kwao ambapo imekuwa ikiwalazimu kuyahama makazi yao
hasa wakati wa kipindi cha masika ambapo maji ya mvua na yale ya kiwanda
huchanganyikana na kujaza uchafu wote majumbani mwao kutoka kiwandani
na kuhatarisha afya zao hivyo kuhamia kwenye nyumba za kulala wageni
kwa muda,hivyo wameiomba serikali kuangalia kwa makini na kuweza kulipatia
ufumbuzi.
Vilevile Mh.Luhaga alifanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda cha
Cement Wazo kilichopo Tegeta wilaya ya kinondoni jijini Dar es salaam,hata
hivyo hakuweza kukutana na kiongozi yeyote wa kiwanda hicho kwa madai
kua walikua nje ya mkoa wa Dar es salaam,aidha Mh.Mpina alitoa tamko
la serikali kuwa,serikali ya awamu ya tano haina uadui na wafanyabiashara
pamoja na wawekezaji kama inavyozaniwa na watu wengine,bali inachotaka
ni kufuatwa kwa Sheria,taratibu na kanuni kama inavyostahili.
EmoticonEmoticon