DC KINONDONI AANZA MAPAMBANO DHIDI YA WATUMISHI HEWA

April 29, 2016

 
NA BASHIR NKOROMO Mkuu wa Wilaya a Kinondoni, Dar es Salaam,  Salum Hapi amesema, Serikali katika wilaya hiyo imebaini kuwa  imepoteza zaidi ya sh. bilioni 1.331 kwa kuwalipa wafanyakazi hewa wapatao 89.hadi sasa.
Amesema, baada ya kuapishwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo siku saba zilizopita, amesimamia maofisa wake kufanya uchunguzi na kubaini kuwa pamoja na wafanyakazi hao hewa ambao wameisababishia serikali kupoteza sh. 1, 331, 734, 881 pia wapo watumishi vivuli wapatao 8823 ambao wanalipwa mishahara wakati  hawafanyi kazi katika maeneo husika kutokana na sababu mbalimbali.
Hapi amesema wafanyakazi hao vivuli ni pamoja na waliohamia idara nyingine lakini wakati wanalipwa huko walikokwenda bado wanalipwa katika idara walizokuwepo mwanzo na kwamba wengi wao wapo katika Idara ya Elimu.
Akzungumza na waandshi wa habari Ofisini kwake, leo, Hapi amesema, amebaini hatua hiyo baada ya kufanya uchunguzi wa kinaa na kuwabinya wasimamizi katika idara mbalimbali za utumishi, na kwamba ameelekeza mwanasheria kuchukua hatua haraka ili wahusika wachukulie hatua za kisheria.
Katika hatua nyingine, Hapi amewataka wafanyabiashara ndogondogo maarufu kwa jina la machinga, kuwa kuanzia kesho ni marufuku kufanya shughuli zao katika maeneo yasiyo mahsusi kwa biashara katika wilaya ya Kinondoni.
Amesema, agizo hilo ni utekelezaji wa agizo la Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda la kutaka ifanyike hivyo kwa lengo la kulifanya jiji liwe safi kuunga mkono agizo la Rais Dk. John Magufuli la kuhimiza usafi nchi nzima.
Hapi amesema, machinga wote kama wahanitaji kufanya biashara zao ni lazima waende katika maeneo yaliyopangwa, ambayo alisema, hapo mengi na bado yana nafasi za kutosha kwa ajili ya kutumika kufanyia biashara.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »