Katibu
wa kamati maalum ya NEC, idara ya itikadi na uenezi CCM Zanzibar Bi,
Waride Bakar Jabu akimkabidhi misaada Katibu mkuu wa ofisi ya makamo wa
pili wa rais, Joseph Abdallah Meza huko kwa ajili ya kuwasaidia wahanga
wa mafuriko waliopo kambi ya mwanakwere “C” Unguja.Katibu
wa kamati maalum ya NEC, idara ya itikadi na uenezi CCM Zanzibar Bi,
Waride Bakar Jabu akimkabidhi misaada Katibu mkuu wa ofisi ya makamo wa
pili wa rais, Joseph Abdallah Meza huko kwa ajili ya kuwasaidia wahanga
wa mafuriko waliopo kambi ya mwanakwere “C” Unguja.
Katibu wa kamati maalum ya NEC, idara ya itikadi na uenezi CCM Zanzibar Bi, Waride Bakar Jabu akikagua wahanga wa mafuriko katika kambi ya mwanakwere zanzibar.
Kambi ya kipindupindu iliyopo chumbuni zanzibar.
…………………………………………………………………………………………………………….
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar.
CHAMA chama cha Mapinduzi (CCM)
Zanzibar kimewataka wananchi kuendelea kufuata kanuni na taratibu
zinazotolewa na wataalamu wa kiafya ili kujikinga na maambukizi ya
maradhi ya kipindupindu yaliyopo nchini.
Wito huo umetolewa na Katibu wa
Kamati Maalum NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Waride
Bakar Jabu katika ziara ya kuwatembelea na kuwafariji wagonjwa wa
Kipindupindu wa kambi iliyopo Chumbuni Zanzibar, alisema endapo
wananchi watafuata kanuni za kiafya itasaidia kutoweka ugonjwa huo kwa
haraka.
Waride alisema CCM itaendelea
kutoa misaada ya hali na mali kwa wagonjwa wa kipindupindu ili kusaidia
serikali huduma za uendeshaji kwa wagonjwa hao.
“ Tunawaomba wananchi waendelee
kuweka mazingira yao katika hali ya usafi sambamba na kutumia maji
salama, vyoo kuwa visafi na wagonjwa wenye dalili za maradhi hayo
kupelekwa haraka katika kambi za kipindupindu.
Pia CCM inawapa pole wananchi
wote waliopata maradhi ya kipindupindu na kuwasihi waendelee kuwa
wavumilivu katika kipindi hiki kigumu cha matibabu yao.”, alisema Bi,
Waride na kuzisihi taasisi zingine za serikali na binafsi kutoa misaada
kwa wagonjwa hao kwani maradhi ya Kipindupindu hayana itikadi za kisiasa
bali yanawapata wananchi wote.
Aliwashauri wanawake nchini ambao
ni walezi wa watoto na mama wa nyumbani kuacha tabia ya kutupa ovyo
pempasi za kuwafungia watoto kwani nazo ni miongoni mwa vitu
vinavyopelekea kuenea kwa maradhi ya kipindupindu nchini.
“ Wanawake tukumbuke kuwa kila
janga lolote sisi pamoja na watoto ndiyo waathirika wa mwanzo hivyo
lazima tuwe makini katika kuweka mazingira yetu katika hali ya usafi
pia tusitupe pempasi ovyo bali tuziweke katika sehemu zinazostahiki.”
Alisisitiza Waride.
Naye Daktari dhamana wa Wilaya ya
Magharibi Unguja ambaye pia ni Mkuu wa Kambi ya Kipindupindu Chumbuni
Zanzibar, Ramadhan Mickdad Suleiman ameshukru msaada uliotolewa na CCM
na kuahidi kuutumia kwa malengo yaliyokusudiwa.
Akitoa takwimu za hali ya
maambukizo ya ugonjwa huo kwa sasa, Mickdad alisema ya hali ya
maambukizo kwa sasa imepungua kutoka wagonjwa 40 kwa siku hadi 21
wanaolazwa katika kambi hiyo.
Alisema hali hiyo imetokana na
utekelezaji wa agizo la Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein
alipowaagiza wananchi wanaofanya biashara za vyakula na vinywaji kuacha
kuuza kwa muda ili kudhibiti kupunguza kasi ya maambukizi ya
kipindupindu.
Alifafanua kuwa mpaka sasa kambi
hiyo tayari imeshapokea wagonjwa 2026 waliopatiwa matibabu na kupona na
wakaondoka na kati ya hao wamefariki wagonjwa 43 mpaka sasa.
“ Tunaishauri jamii kudumisha
usafi wa vyoo na kula vyakula na maji vilivyokuwa salama kwani ugonjwa
huu unaambukizwa kwa kasi katika maji ya kunywa yenye bakteria wa
kipindupindu ama kumgusa maiti yaliyekufa kwa ugonjwa au kugusana na
mtu aliyeambukizwa kipindupindu.”, alisema Bi, Micjdad.
Aliwaomba wananchi wenye uwezo
pamoja taasisi binafsi na serikali kutoa misaada kujitokeza kutoa
misaada mbali mbali ya kuwasaidia wagonjwa wa maradhi hayo waliopo
katika kambi hiyo.
Mapema Waride alitembelea na
kuwafariji Wahanga wa mafuriko waliopo katika kambi ya Shule ya
Mwanakwerekwe “ C” Unguja, aliwapa pole kwa matatizo yaliyowafika na
kuwaomba waendelee kuwa wavumilivu katika kambi hili huku serikali
ikiendelea kutafuta mbinu za kuwasaidia ili wapate makaazi katika sehemu
salama.
Alitoa wito kwa wananchi
wanaoishi katika sehemu za mabonde na sinazojaa maji wakati wa msimu wa
mvua za maska kuhama haraka kabla hawajapata athari za kukumbwa na
mafuriko hayo.
Kwa upande wake Katibu mkuu wa
Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar, Joseph Abdallah Meza alitoa
shukrani kwa uongozi wa CCM kwa msaada wao wa kuisaidia kambi hiyo yenye
wananchi zaidi 400.
Alisema serikali bado inaendelea
kuwahudumia wananchi hao ambao wamepata maafa ya mafuriko na kupoteza
makaazi yao hivyo bado panahitajika misaada mbali mbali ya maji na
vyakula pamoja na huduma za kibinadamu.
Misaada iliyotolewa na CCM katika
ziara hiyo ina thamani zaidi ya shilingi milioni tano (5) kwa upande
wa kambi ya kipindupindu Chumbuni ni pamoja na Maji ya kunywa, Dawa za
Chroline, Sabuni za kufulia na kuogea, viatu vya mvua, dawa ya choo na
mashine za kufukizia dawa Sprayers.
Vingine vilivyotolewa katika
kambi ya wahanga wa mafuriko iliyopo Mwanakwere “C” ni pamoja na
Pempasi za watoto, maji ya kunywa, sabuni za kuogea na kufulia, sabuni
za chooni na madaftari ya wanafunzi.
EmoticonEmoticon