Mkuu wa Shule ya Sekondari Shimbwe iliyopo wilayani Moshi vijijini,Jacob Costantine akimueleza jambo Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kaksakazini,Henry Tzamburakis alipofika shuleni hapo kwa ajili kukabidhi mashine ya kisasa ya kuduru karatasi.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
KAMPUNI ya
Mawasiliano ya simu za mkononi ya Vodacom imekabidhi kwa shule ya sekondari ya
Shimbwe iliyopo wilaya ya Moshi vijijini ,msaada wa mashine yenye uwezo wa
kufanya kazi zaidi ya tatu ikiwemo kudurusu karatasi.
Msaada wa mashine
hiyo (Photocopier) yenye thamani ya zaidi ya sh Mil 12 ni sehemu ya msaada wa
vifaa mbalimbali ambavyo kampuni hiyo kupitia mradi wa “Pamoja na Vodacom”
imekabidhi shuleni hapo zikiwemo Kompyuta mpakato 30.
Mbali na msaada wa
Kompyuta na Mashine hiyo kampuni hiyo pia ilitoa wataalamu kutoka shirika
lisilo la kiserikali la Learning in Sync
kwa ajili ya kuweka program maalumu katika kmpyuta za kufundishia na kujifunzia
.
Mkuu wa Vodacom
Kanda ya Kaskazini,Henry Tzamburakis alisema kutolewa kwa mashine hiyo ni
muendelezo wa msaada ambao Vodacom kupittia mradi wa Pamoja na Vodacom
imeendelea kutoa kwa nchi nzima.
“Huu ni muendelezo
wa msaada ulitolewa awali ,Kampuni ya Vodacom tunarudisha sehemu ya faida kwa
wananchi na wateja wetu,pamoja na hayo ni kusaidia wadogo zetu kuingia katika
digitali wakiwa na umri mdogo na kuwaandaa na maisha ya baadae,”alisema
Tzamburakis.
Alisema Mashine
hiyo ya kisasa itasaidia kupunguza changamoto zilizokuwa zikiikabili shule hiyo
hususani katika maandalizi ya mitihani pamoja na machapisho mengine ambayo
shule ili lazimika kuingia gharama kubwa kuchapisha.
Katika kuhakikisha
walimu wa shule hiyo wanaweza kutumia vyema mashine hiyo Tzamburakis alisema
ofisi ya Vodacom kanda ya Kaskazini itatoa mtaalamu kwa ajili ya kufundisha
namna ya kuitumia.
“Ofisi ya kanda ya
Vodacom ina wataalamu wa IT ambao watasaidia katika kutoa mafunzo kwa walimu ya
namna ya kutumia mashine hizi na tutaweka utaratibu wa kufika mara moja kwa
mwezi katika shule hii ili waweze kubadilishana uzoefu na walimu wa masomo hayo.”alisema
Tzamburakis.
Kwa upande wake
mkuu wa shule ya sekondari Shimbwe,Jacob Costantine aliishikuru kampuni ya
Vodacom kwa msaada huo huku akieleza changamoto zilizoikabili shule hiyo
ikiwemo ya kuchapisha mitihani kwa gharama kubwa .
“Tumepewa mashine
ya Photocopy ikiwa ni ahadi ya mgeni rasmi kutoka Vodacom baada ya kumueleza
kuwa tumekuwa tukitumia gharama kubwa hasa kipindi cha mitihani ,kuchapisha
mitihani yetu ya mihula na ile ya mwisho wa mwaka”alisema Costantine.
Alisema kupatikana
kwa mashine hiyo ,sasa shule itakuwa na uwezo mkubwa wa kuchapisha machapisho
mbalimbali vikiwemo vitabu ambavyo upatikanaji wake umekuwa mgumu kwa ajili ya
wanafunzi hao kujifunzia.
Mkuu huyo wa shule
alisema wamekuwa wakitumia zaidi ya shilingi Milioni nne kwa ajili ya
maandalizi ya mitihani shulebi hapo na kwamba kwa sasa adha ya kuandika ubaoni
mitihani ya majaribio itatoweka.
Mwisho.
EmoticonEmoticon