Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akifungua Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akifungua Mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam
Februari 9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
kaipata maelezo kutoka kwa Bi Fatuma Kango kuhusu Msimbomilia au
Barcode baada ya kufungua Mkutano wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar
es slaam Februari 9, 216. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akiagana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Sekta Binafisi nchini, Reginald Mengi baada ya kufungua
mkutano wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi kwenye Kituo cha
Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari
9, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
akimsikiliza Rais wa VICOBA, Devota Likokola (wapili kulia ) wakati
alipotembelea banda la Benki ya Posta Tanzania katika Mkutano wa Wadau
wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi alioufungua kwenye Kituo cha Kimataifa
cha Mikutano cha walimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam Februari 9,
2016. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu)
…………………………………………………………………………………………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amesema Serikali imebuni na kuanza kutekeleza Sera ya Uwekezaji ili
kufikia lengo la kuwawezesha wananchi kiuchumi.
“Taarifa zilizopo zinaonyesha ni
asilimia 10 tu ya Watanzania ndio wanaomiliki uchumi wa nchi na sera
hiyo ndiyo inatoa mwongozo wa jumla unaohakikisha kwamba wananchi
wanapata fursa mbalimbali za kiuchumi ambazo zitawawezesha kujenga na
kufaidika na uchumi wa mchi yao,” alisema.
Waziri Mkuu amesema maeneo
yanayolengwa na sera hiyo ni yale yenye kuleta matokeo ya haraka na
yanayogusa maisha ya wananchi hasa katika sekta za kilimo, ufugaji,
uvuvi, misitu, ujenzi, biashara, utalii, madini, viwanda na
usafirishaji.
Ametoa kauli hiyo leo mchana
(Jumanne, Februari 7, 2016) wakati akizungumza na washiriki wa Mkutano
wa Kwanza wa Wadau wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi nchini uliofanyika
kwenye ukumbi wa kituo cha kimataifa cha mikutano cha mwalimu Nyerere,
jijini Dar es Salaam.
Alisema Dira ya Taifa ya
Maendeleo 2025 inalenga kuhakikisha kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa nchi
yetu inamilikiwa na Watanzania wenyewe. Waziri Mkuu pia alizindua
Mwongozo wa Utekelezaji Mkakati wa Taifa wa Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi.
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu
kufungua mkutano huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Ajira na Walemavu, Bibi Jenista Mhagama alisema hadi sasa mikoa
20 imekwishatenga maeneo ya uwekezaji kwenye halamhashauri zake na
imeanza kuweka miundombinu ya kuvutia wawekezaji.
Naye Mweyekiti wa Baraza la Taifa
la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, Prof. Omari Issa alisema katika dunia
ya sasa imebainika kuwa haina maana kumpatia mtu mkopo bila kumtafutia
masoko au kumuunganisha wadau wa masoko. Kwa hiyo wamejipanga kuwasaidia
Watanzania kwa kuwaunganisha na masoko.