
Taarifa zilizotufikia zinasema kuwa Kivuko cha mto Kilombero mkoani Morogoro kimezama kikiwa na abiria zaidi ya 30 na magari 3.


Mkuu wa wilaya ya Kilombero Bw Leph Gembe amethibitisha
kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa, kuzama kwa kivuko hicho
kulichangiwa na upepo mkali uliokuwa ukivuma wakati huo hivyo kupoteza
uelekeo wake.
Alisema ajali hiyo imetokea jana Majira ya saa 1 usiku wakati kivuko hicho kikitokea Ulanga.
Mkuu
huyo wa wilaya amesema taarifa alizopewa ni kwamba kivuko hicho
kilikuwa na abiria 30 na wote waliokolewa baada ya kupewa majaketi ya
usalama baada kivuko hicho kuanza kupoteza uelekeo kutokana na upepo
mkali.
Hata hivyo amesema kuna mashaka ya mtu mmoja kuwa alizama na wanaendelea kufuatilia kupata ukweli wake.
Ameyataja magari yaliyozama kuwa ni pamoja na gari moja la CRDB, gari la kampuni ya mitiki, fuso moja pamoja na bajaji.

Muonekano wa Misingi ya Daraja la Mto huo, huku kivuko kilichozama kikionekana kulia.
EmoticonEmoticon