Tigo yagawa simu 200 kwenye “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake” Rufiji

December 28, 2015
Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas, akiongea na waandishi wa habari na kinamama wa wilayani Rufiji waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali na utunzaji wa mazingira programu ijulikanayo “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”. Wengine kulia kwake ni John Kikomo Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET) na kushoto kwake ni  Dkt. Flora Myamba Mkurugenzi Mtafiti Kinga Jamii toka REPOA.


Mkurugenzi Mtafiti Kinga Jamii toka REPOA, Dkt. Flora Myamba akiongea na waandishi wa habari na kinamama wa wilayani Rufiji waliohudhuria mafunzo ya ujasiriamali na utunzaji wa mazingira programu ijulikanayo “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”. Wengine toka kushoto John Kikomo Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET) na Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas
Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas akimkabidhi simu Bi.Habiba Mtigino kutoka kijiji cha Umwe wilayani Rufiji. Jumla ya simu 200 zilitolewa na Kampuni ya Tigo kwa Wanawake wasiokuwa na uwezo wa kununua simu wilayani humo kupitia mpango unaojulikana kama, “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”



Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa mazingira(JET), John Kikomo akionyesha kimoja kati ya vyeti watakavyopewa kinamama  walioshinda shindano la kutunza mazingira wilayani Rufiji. Mpango huo ulidhaminiwa na Tigo na asasi tatu zisizo za serikali za REPOA, KIDOGO KIDOGO na Care International.  




 Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas akimkabidhi simu Bi.Mozza Salum kutoka kijiji cha Umwe wilayani Rufiji. Jumla ya simu 200 zilitolewa na Kampuni ya Tigo kwa Wanawake wasiokuwa na uwezo wa kununua simu wilayani humo kupitia mpango unaojulikana kama, “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake”





Baadhi ya kinamama wa wilayani Rufiji Mkoani Pwani waliohuduria mkutano wa mradi wa Kuwaunganisha Wanawake wenye lengo la kujifunza ujasiriamali na kutunza mazingira wakifuatilia kwa makini, Kampuni ya Tigo ndio mdhamini wa mradi huo.


Baadhi ya kinamama wa wilayani Rufiji Mkoani Pwani waliohuduria mkutano wa mradi wa Kuwaunganisha Wanawake wenye lengo la kujifunza ujasiriamali na kutunza mazingira wakifuatilia kwa makini, Kampuni ya Tigo ndio mdhamini wa mradi huo.



  

  • Itashirikana na  REPOA, CARE INTERNATIONAL & KIDOGO KIDOGO

Rufiji, Desemba 23, 2015: Tigo imetoa simu za mkononi 200 ambazo zitasambazwa kwa wanawake maskini ambao hawana uwezo wa kununua simu katika wilaya ya Rufiji mkoani Pwani, lengo kuu likiwa ni kuziba pengo la kijinsia katika umiliki wa simu Tanzania.
Usambazaji wa simu hizo upo chini ya programu inayojulikana, “Mradi wa Kuwaunganisha Wanawake” utafanyika kwa kushirikiana na asasi tatu zisizo za serikali za REPOA, KIDOGO KIDOGO na Care International.  
Akizungumzia zoezi hilo Meneja Huduma kwa Jamii wa Tigo, Bi. May Thomas, alisema kwamba mtazamo wa Tigo uko kwenye sera za kampuni ya kuwawezesha watu walio na kipato duni ndani ya jamii katika kuzipata simu za mkononi.
“Tigo  inadhamiria kuboresha muunganisho wa simu za mkononi nchini Tanzania  hususani miongoni mwa wanawake  ambao kimsingi wana uwezo mdogo wa kupata simu,” alisema Bi.Thomas na kuongeza, “Ni matumaini yetu kwamba  kwa kusambaza simu hizi kwa wanawake maskini katika wilaya ya Rufiji, Tigo itakuwa imechangia kupunguza  pengo la kijinsia katika umiliki wa simu nchini.”
 Thomas alisema kwamba Tigo imewekeza zaidi ya dola 30,000 ambazo zitatumika kusambaza  pamoja na kuangalia tathmini ya matokeo ya mradi. Aliongeza kwamba washirika watatu REPOA, CARE International na KIDOGO KIDOGO kwa pamoja wataongoza utekelezaji huo wa usambazaji wa simu kwa kutoa laini ya simu pamoja na kufanya tathmini ya matokeo ya mradi.
“Pengo lililopo la kijinsia katika kuifikia teknolojia ya simu linaweza kukwaza Tanzania katika mchakato wa kufikia Malengo ya Maendeleo ya Milenia katika kukuza usawa kijinsia na kuwawezesha wanwake nchini na ndio maana Tigo inachukua hatua za kuunga mkono mradi huu,” alisema Bi.Thomas.
 Kwa mujibu wa Bi. Thomas mradi huo unalenga kuwanufaisha watu 500 katika kipindi cha mwaka 2015 na 2016 na inakuwa ni mara ya pili kwa Tigo  kusambaza simu za mkononi kwenye mkoa huo kwani mara ya kwanza ilikuwa amwaka 2014. 


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »