Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi Prof. Idrisa Mshoro akimkabidhi cheti
mmoja wa wanafunzi wa mwaka wa nne aliyefanya vizuri katika masomo yake
kwa mwaka 2014/2015 wakati wa leo jijini Dar es salaam.
Naibu
Makamu Mkuu wa Chuo anayeshughulikia masuala ya Taaluma wa Chuo Kikuu
cha Ardhi Prof. Gabriel Kassenga akizungumza na wanafunzi na wageni
mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa Tuzo kwa wahitimu wa chuo
hicho waliofanya vizuri leo jijini Dar es salaam.
Baadhi
ya Wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Ardhi, wawakilishi wa Makampuni na
Taasisi mbalimbali waliochangia tuzo mbalimbali na Wahitimu wa miaka ya
nyuma wa Chuo hicho wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla fupi
ya utoaji wa Tuzo kwa wanafunzi waliofanya vizuri leo jijini Dar es
salaam.
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Ardhi waliofanya Vizuri waendelea kupokea
tuzo zao. Takribani wanafunzi 126 wamepata Tuzo na zawadi mbalimbali
wakiwemo wanafunzi kike 61 waliofanya vizuri katika masomo ya Sayansi.
Wanafunzi na Wageni mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo
Mwanafunzi
Bora wa Kike wa Chuo Kikuu cha Ardhi katika fani ya Upimaji wa Ardhi (
Geomatics) Bi. Lilian Kato akipokea zawadi yake ya mashine ya kupimia
Ardhi (Total Station) yenye thamani ya shilingi milioni 15 aliyozawadiwa
na Kampuni ya High Tech Systems kwa kuwa mwanafunzi bora wa kike wa
mwaka wa nne kwa mwaka 2014/2015.
Mwanafunzi
wa mwaka wa 4 wa Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU) Bi. Beatrice Kaijage
akipokea zawadi yake kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya High Tech
System ya jijini Dar es salaam.
Mwanafunzi
Bora wa Kike wa Chuo Kikuu cha Ardhi katika fani ya Upimaji wa Ardhi (
Geomatics) Bi. Lilian Kato akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo
pichani) namna atakavyonufaika na
mashine ya kupimia Ardhi (Total Station) aina ya Stonex aliyozawadiwa na
Kampuni ya High Tech Systems kwa kuwa
mwanafunzi bora wa kike wa mwaka wa nne kwa mwaka 2014/2015.
Viongozi
wa Wakuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi wakiwa katika picha ya pamoja na
wahitimu wa miaka ya nyuma wa Chuo hicho, viongozi wa taasisi na
Makampuni mbalimbali mara baada ya hafla ya utoaji wa tuzo iliyofanyika
leo jijini Dar es salaam.
Viongozi
wa Wakuu wa Chuo Kikuu cha Ardhi wakiwa katika picha ya pamoja na
wanafunzi wa chuo hicho waliofanya vizuri kwa mwaka 2014/2015 , wahitimu
wa miaka ya nyuma wa Chuo hicho, viongozi wa taasisi na Makampuni
mbalimbali mara baada ya hafla ya utoaji wa tuzo na zawadi mbalimbali
iliyofanyika leo jijini Dar es salaam. Picha/Aron Msigwa.
EmoticonEmoticon