Katibu
wa Kamati ya Taifa Stars, Teddy Mapunda leo amefanya makutano na
waandishi wa habari katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume,
ambapo ametumia nafasi hiyo kutangaza namba za simu za uchangiaji kwa
Watanzania kwa ajili ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
Akiongea na waandishi wa habari,
Teddy amesema watanzania wanaweza kuichangia Taifa Stars kiasi chochote
cha fedha kuanzia shilingi mia moja (TZS 100) kwenda namba 0654-888868
(Tigo Pesa) na 0789-530668 (Airtel Money) ambazo zitatumika kwa ajili ya
motisha kwa wachezaji, uhamasishaji/masoko na maboresho ya kambi za
ndani na nje ya nchi.
Aidha Teddy amesema Kamati ya
Taifa Stars inaandaa utaratibu kwa ajili ya washabiki watakaotaka
kusafiri kuelekea nchini Algeria katika mchezo wa marudiano, waweze
kuchangia gharama za usafiri ili waweze kwenda kuipa sapoti Stars katika
mchezo wa marudaiano Novemba 17, 2015.
“KamatI inaendelea na mchakato wa
kukamilisha suala la kambi ya Taifa Stars, na mpaka sasa tunasubiri
majibu kutoka katika vyama vya soka vya vya nchi tunazotaka kuweka kambi
ambazo ni Afrika Kusini, Dubai na Oman kabla ya kutangaza rasmi kambi
itakapokuwa” Alisema Teddy.
Kamati inawaomba watanzania,
wadau, washabiki na wapenzi wa mpira miguu nchini kuichangia timu ya
Taifa kupitia namba zilizotolewa na pia kujitokeza kwa wingi kuujaza
uwanja wa Taifa siku ya mchezo wa tarehe 14 Novemba, 2015
EmoticonEmoticon