Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi
ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa klabu ya Simba, Evans Aveva
kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa kiongozi wa klabu hiyo Emmaneul Makaidi
aliyefariki Dunia jana mkoani Lindi.
Katika salam zake, Malinzi amewapa pole wafiwa, ndugu, jamaa,
marafiki, wapenzi wa klabu ya Simba pamoja na wadau wa mpira wa miguu
nchini, kufuatia kifo hicho cha kiongozi huyo.
Marehemu Emmanuel Makaidi alipata kuwa kiongozi wa klabu ya Simba
1960-1970 katika nafasi mbalimbali zikiwemo nafasi za Katibu mwenezi,
Katibu Mkuu na kukaimu Uenyekiti wa klabu ya Simba kabla ya kujiunga na
masuala ya kisiasa.
Kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini na watanzania, TFF
inawapa pole wafiwa na kuwatakia faraja katika kipindi hichi cha
maombelezo.
EmoticonEmoticon