RC MPYA TANGA ATEMA CHECHE

September 19, 2015



Tangakumekuchablog

MKUU wa Mkoa wa Tanga aliehamishiwa Mkoa wa Rukwa, Said Magalula, amemtisha zigo la migogoro ya ardhi aliyodai kufanya na watendaji wa Idara ya Mipango miji  mbadala wake , Mwantumu Mahiza aliehamia Tanga.

Akimkaribisha  Leo  ukumbi wa ofisi ya mikutano jengo la Mkuu wa Mkoa, Magalula alisema migogoro ya ardhi inasababishwa na watendaji wa mipango miji na sio wananchi hivyo kumuachia zigo hilo ambalo limekuwa likiwatesa wananchi.

Alisema Idara hiyo imekuwa ikiwagombanisha wananchi wenyewe kwa wenyewe  pasina sababu na linapobumbuluka hutoa visingizio vya sheria na mwaka hivyo kumtaka kulivalia njuga ikiwa na pamoja na kulikomesha.

“Mheshimiwa dada yangu Mwantumu Mahiza karibu Tanga na niwaage watu wa Tanga kwa kusema kwaherini-----ila kuna jambo moja ambalo niseme waziwazi pasina kuoneana haya kuwa Idara ya mipango miji ni mabingwa wa kugombanisha wananchi” alisema Magalula na kuongeza

“Wao ndio wanaofanya hiyana kwa kufanya mavirigisa na ujanja ujanja halafu husikilizia----pale linapobumbuluka hukaa pembeni kisha kutoa vifungu vya sheria na mwaka baada ya watu kugombana kuhamasiana” alisema

Alimtaka Mkuu huyo mpya kulikomesha tatizo hilo ambalo kwa muda mrefu limekuwa likirudisha nyuma maendeleo ya wananchi badala ya kufanya kazi za maendeleo wamekuwa wakipanga foleni ofisi za mipango miji ambako ndiko kiini cha tatizo.

Akizungumza baada ya makabidhiano, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza, alisema hatomuonea huruma kiongozi yoyote katika kazi bila kujali cheo wala nasaba hivyo kuwataka kuwatumikia wananchi kwa haki na uwazi.

Alisema yote ambayo ameelezwa na mtangulizi wake atayafanyia kazi na yule ambaye amefanya madudu ajisafishe kabla ya operesheni katika ofisi na idara hajaianza.

“Mheshimiwa Magalula changamoto na kero zote ambazo umeniambia hapa mbele ya wakuu wa idara na watendaji ofisini nimezipokea na niko tayari kwa lolote kwani uwezo ninao” alisema Mahiza

Alisema kinachotakiwa ni kufanya kazi kwa uwazi na uwajibikaji ili kuwaletea maendeleo wananchi na kudai kuwa yeyote ambaye ataonyesha ukiukwaji wa maadili ni vyema akajiengua mapema.


Mkuu wa Mkoa mpya wa Tanga, Mwantumu Mahiza, akizungumza na wakuu wa Wilaya, Wakuu wa Idara na  Taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na viongozi wa vyama vya siasa mara baada ya makabidhiano na mtangulizi wake aliehamishiwa Mkoa wa Katavi.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »