IGP MANGU AZINDUA NA KUKAGUA MIRADI YA POLISI TABORA, TANGA NA SINGIDA

July 09, 2015

7
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akizungumza na wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama mkoani Tabora wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe.Ludovick Mwananzila na Mkuu wa Wilaya ya Tabora Mhe.Suleiman Kumchaya.
(Picha na Frank Geofray-Jeshi la Polisi).
2
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Wodi ya wazazi katika Zahanati ya Polisi Tabora wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.Kulia ni Mganga Mkuu wa mkoa wa Tabora.IGP pia alitumia ziara hiyo kuzungumza na Maafisa, wakaguzi na Askari wa mkoa huo.
3
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akiwa na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Polisi Dkt.Nyanda wakitoka kukagua Wodi ya wazazi katika Zahanati ya Polisi Tabora baada ya kuizindua wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo..IGP pia alitumia ziara hiyo kuzungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa mkoa huo.
4
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akiweka jiwe la msingi katika jengo la Kikosi cha usalama barabarani mkoani Tabora wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo ambapo pia alitumia ziara hiyo kuzungumza na Maafisa, Wakaguzi na Askari wa mkoa huo.Kulia ni Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Kamishna msaidizi wa Polisi, Juma Bwire.
5
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu akikagua ujenzi unaoendelea wa Kituo cha Polisi na Makazi ya Askari Wilayani Ikungi mkoani Singida wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.Katikati ni ni kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi wa Polisi Thobias Sedoyeka na Mkuu wa Polisi wa wilaya ya Ikungi.
6
Kamanda wa Kikosi cha Ujenzi cha Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi mwandamizi wa Polisi, Richard Malika akimtembeza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu kuangalia ujenzi wa kituo cha Polisi wilayani Lushoto mkoani Tanga wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika mkoa huo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »