UMOJA WA MATAIFA WAIBUKA KIDEDEA KATIKA UHABARISHAJI NA UTOAJI ELIMU KWENYE TUZO ZA MAONYESHO YA 39 YA SABASABA

July 04, 2015
  DSC_0178
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkadhi Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) cheti na tuzo katika kipengele cha Uelimishaji bora kupitia Uandishi wa machapisho na mpangilio bora wa maonyesho, baada ya Umoja wa Mataifa kuibuka mshindi wa kwanza katika maonyesho ya 39 ya kimataifa ya biashara ya Sabasaba yalipozinduliwa rasmi. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tan Trade), Jacqueline Mneney Maleko (kushoto) pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Dkt. Abdallah Kigoda (kulia).
DSC_0179 FullSizeRender_2
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaohudumia banda hilo kwenye maonyesho ya Sabasaba wakisheherekea mara baada ya kutwaa tuzo hiyo.
UN Tanzania inawakaribisha Watanzania wote wanaotembela maonyesho sabasaba kufika katika banda lao lililopo Karume Hall na kuweza kushiriki kutoka maoni ya juu ya utendaji wa kazi za Umoja wa Mataifa Tanzania kwa njia ya mtandao wa simu yako bila kutozwa malipo yoyote ukitumia huduma hiyo, kwa wateja wote mitandao ya Airtel, Tigo na Vodacom.
Jinsi ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi (SMS), kwa kuandika neno UN au UMOJA WA MATAIFA ambapo kwa watumiaji wa mtandao wa Airtel watatuma ujumbe wao kwenda namba 15453, kwa watumiaji wa mtandao wa Tigo wanatuma kwenda 15055 au 15453 na kwa Vodacom ni namba 15055.
Njia nyingine ya kuwasilisha maoni yako moja kwa moja kupitia mtandao (Online) bofya link hii http://gpl.cc/UN2
FullSizeRender  

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »