“WAMBURA: TUZO IMENIPA MZUKA WA KUFANYA VIZURI MSIMU UJAO”

May 10, 2015
KIUNGO wa Timu ya Coastal Union, Godfrey Wambura amesema kuwa tuzo ya uchezaji bora ya mwezi wa February aliyoipata imempa mzuka wa kuhakikisha anajipanga imara ili kuendelea kufanya vizuri.

Wambura ambaye alijiunga na Coastal Union katika drisha dogo akitokea klabu ya Kagera Sugar alisema hayo juzi mara baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo pamoja na hundi ya sh.milioni moja kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo Vodacom.

Akizungumza jana, Wambura alisema kuwa anaamini uteuzi huo wa uchezaji bora uliofanywa na bodi ya Ligi kuu ulikuwa makini na ndio maana umeweza kumuwezesha kupata nafasi hiyo ambayo alikuwa akiiwaza kwa kipindi cha muda mrefu.

   “Tuzo hii imenipa hamasa ya kuhakikisha ninatumia vizuri nafasi yangu kama mchezaji lengo likiwa kuipa mafanikio timu yangu hasa katika harakati za kucheza ligi kuu kwa ufanisi mkubwa “Alisema Wambura.

Hata hivyo aliwataka wachezaji wengi kujituma na kucheza mechi kwa juhudi kubwa ili kuweza kupata nafasi za kuwawezesha kuonekana na kuchaguliwa kuwa wachezaji bora kama ilivyokuwa kwake.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »