TAASISI ya
kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mambo ya mikopo
kwa watumishi wa wa umma na kampuni zilizoidhinishwa, mwishoni mwa wiki
ilizindua tawi lake jipya la 80 wilayani Ileje, mkoani Mbeya, huku Mkuu
wa wilaya hiyo, Rosemary Staki Senyamule, akiwataka wananchi wake
kukopa kwa sababu maalum.
Mkuu
wa Wilaya ya Ileje, Mheshimiwa Rosemary Senyamule kulia, akionyeshwa
nyaraka za ofisi ya Taasisi ya Kifedha ya Bayport Financial Services,
inayojihusisha na mambo ya mikopo katika uzinduzi wa taasisi hiyo katika
wilaya hiyo ya Ileje, mkoani Mbeya. Kushoto ni Meneja wa Kanda ya
Nyanda za Juu Kusini, Alpha Akim. Uzinduzi huo ulifanyika mwishoni mwa
wiki iliyopita na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wilayani humo.
Kufunguliwa
kwa tawi hilo si kutainua uchumi wa wananchi wa Ileje watakaotumia
fursa ya uwapo wa ofisi hiyo, bali pia kutarahisisha utoaji wa huduma wa
taasisi hiyo ya Bayport nchini Tanzania.
Wageni
mbalimbali wakiangalia shughuli za uzinduzi wa tawi jipya la taasisi ya
kifedha ya Bayport Financial Services, wilayani Ileje, mkoani Mbeya,
mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya
hiyo, Rosemary Senyamule.
Akizungumza
katika uzinduzi wa tawi hilo jipya, Mkuu huyo wa wilaya Ileje, Rosemary
alisema kuwa wananchi wakiitumia fursa ya tawi hilo kutainua pia
kiwango cha uchumi cha watu wake.
Baadhi
ya wageni waalikwa wakisoma vipeperushi vya taasisi ya kifedha ya
Bayport Financial Services, wilayani Ileje, mkoani Mbeya.
Alisema
suala la mikopo ni jambo jema kutokana na uwezo mzuri unaoweza
kuwaendeleza wananchi, wakiwamo watumishi wa umma na wafanyakazi wa
kampuni zote zilizoidhinishwa, ambao kimsingi ni watu wanaotakiwa
kuendelezwa kwa mambo mengi.
Meneja
wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wa Bayport Financial Services, Alpha
Akim, akizungumza jambo katika uzinduzi wa tawi lao la 80 wilayani
Ileje, mkoani Mbeya, mwishoni mwa wiki iliyopita na kuhudhuriwa na watu
mbalimbali.
“Kwanza
nawapongeza mno wenzetu wa Bayport Financial Services kwa kuamua kuja
kufungua tawi hapa katika wilaya yetu ya Ileje, ila ni muhimu wananchi
kukopa kwa sababu maalum ili waweze kuendeleza maisha yao kwa kutumia
vyema fursa za mikopo Tanzania.
“Tukifanya
hivyo tunaweza kupata maisha bora kwa sababu tutajimudu kiuchumi, hivyo
ni wakati wetu kufurahia kuanzishwa kwa huduma za taasisi hii hapa
kwetu ileje, maana ndio kwanza wanafungua tawi lao hapa,” alisema.
Naye
Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Alpha Akim, alisema kufungua
kwa tawi hilo pia ni sehemu ya kutoa ajira kwa vijana sanjari na
kuongeza kipato kwa watumishi wa umma na wafanyakazi wa kampuni
zilizoidhinishwa kwa kupitia fursa nzuri ya mikopo.
“Watu
mbalimbali watapata mwangaza mzuri wa kiuchumi wakiwamo wale
watakaopata nafasi ya kufanya kazi nasi, hususan ile ya uwakala, bila
kusahau wale watakaokopeshwa bila amana wala dhamana.
“Naomba
wananchi na wakazi wa Ileje watumie vyema fursa ya uwapo wa taasisi hii
wilayani kwao kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wote kwa pamoja
tunafanikisha kwa vitendo ndoto ya kukuza uchumi wetu na wa Tanzania kwa
ujumla,” alisema Akim, Meneja wa Nyanda za Juu Kusini wa Bayport.
Bayport
Financial Services ni taasisi ya kifedha inayojihusisha na utoaji
mikopo mbalimbali kama vile fedha taslimu, mikopo ya bidhaa, bima ya
elimu kwa uwapendao, ambapo mikopo hiyo inaweza kutolewa ofisini au kwa
njia rahisi ya mtandao wa www.kopabayport.co.tz.
EmoticonEmoticon