Shirikisho
la Mpira wa Miguu nchini TFF limetangaza viingilio vya mchezo kati ya
timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake (Twiga Stars) dhidi ya timu ya
Taifa ya Zambia (She-Polopolo) kiingilio cha juu sh.5,000 kwa VIP na sh.
2,000 kwa majukwaa yaliobakia, mechi hiyo itachezwa ijumaa jioni saa 10
kwenye dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam
Twiga Stars chini ya kocha mkuu
Rogasian Kaijage imeendelea kujifua katika hosteli za TFF zilizopo
Karume, kuhakikisha inaibuka na ushindi katika mchezo huo wa kuwnaia
kufuzu kwa Michezo ya Afrika nchini Congo- Brazzavile mwezi Septemba
mwaka huu.
Katika mchezo wa awali uliofanyika
wiki tatu zilizopita jijini Lusaka nchini Zambia, Twiga Stars iliibuka
na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya wenyeji Zambia, hivyo katika mchezo wa
ijumaa kuhitaji ushindi wa aina yoyote tu ili kuweza kufuzu kwa fainali
hizo.
TFF inawaomba wapenzi, wadau na
washabiki wa mpira wa miguu nchini, kujitokeza kwa wingi siku ya ijumaa
jioni uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuja kuwapa sapoti Twiga
Stars watakapokuwa wanapeperusha bendera ya Taifa.
Wakati huo huo, timu ya Taifa ya
Wanawake ya Zambia (She-Polopolo) inatarajiwa kuwasili usiku wa saa 7.25
kuamkia alhmisi kwa shirika la Ndege la Ethiopia wakiwa na msafara wa
wachezaji 18 na viongozi saba na watafikia katika hoteli ya Tansoma
iliyopo eneo la Gerezani Kariakoo.
Msafara wa Zambia (She-Polopolo)
unaongozwa na mkuu wa msafara Lenny Khuwa, kocha mkuu Albert Kachinga,
kocha msaidizi Kape Saili, kocha wa magolikipa Yona Phiri, daktari wa
timu James Nyimbili, mchua misuli Conerlia Chazura, na meneja wa timu ni
Besa Chibwe
Wachezaji wanaotarajiwa kuwasili
ni Rachel Nachula, Annie Kibanji, Chiko Nkhoma, Osala Kaleo, Joana
Benai, Meya Banda (Nahodha), Misozi CR Chisamu, Jane Nshika Chalwe,
Milika Limwanya, Mary Wilombe, Grace Chanda, Barbra Banda, Memory
Mwaseba, Hazel Natasha Nali, Martha Tembo, Mary Mwakapila na Ireen Lungu
Kesho jioni She-Polopolo wanatarajiwa kufanya mazoezi katika uwanja wa Taifa, uwanja ambao ndio utakaotumika kw amchezo huo.
Waamuzi wa mchezo huo kutoka
nchini Uganda wanatarajiwa kuwasili leo mchana ambao ni Ms Anna Akoyi ,
Ms Nakkito Nkumbi , Ms Jane Mutonyi, na Ms Nabikko Ssemambo, Kamishina
wa mchezo Ms Nomsa Jacobeth Mhalangu kutoka nchini Afrika Kusini
anatarajiwa kuwasili leo jioni.
TFF YAMPONGEZA TENGA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu nchini TFF Jamal Malinzi, amempongeza Bw Leodgar Tenga kwa
kuchaguliwa kuendelea kuwa mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la
Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF).
Aidha Rais Malinzi ametuma salamu
za pongezi kwa wajumbe waliochaguliwa kuwa wajumbe wapya wa Shirikisho
la Mpira wa Miguu baranai Afrika (CAF) na Shirikisho la Mpira wa Miguu
Duniani FIFA.
Katika salamu hizo na nakala zake
kutumwa kwa Rais wa CAF Bw. Issa Haytou na Rais wa FIFA Bw. Blatter,
Malinzi amewatakia kila la kheri katika majukumu hayo mapya,na kwa
ajili ya maendeleo ya mpira wa miguu duniani.
Tenga amechaguliwa nafasi hiyo
baada ya kuwa mgombea pekee kutoka kanda ya Afrika Mashariki
aliyejitokeza kuwania nafasi hiyo na kuungwa mkono na nchi zote
wanachama wa CECAFA.
NB: Kesho alhamisi saa 5 kamili
asubuhi kutakua na mkutano na waandishi wa habari katika Ukumbi wa
Mikutano wa TFF uliopo Karume, makocha wa Twiga Stars na She-Polopolo
wataongelea maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa siku ya ijumaa.
EmoticonEmoticon