Waziri
wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu akiwa na Waziri wa Biashara
na Utalii wa Kenya Bibi Phylis Kandie mara baada ya mazungumzo yao.
Mh.
Waziri Nyalandu akihojiwa katika banda la Tanzania na mwandishi wa
habari wa kituo cha Televisheni cha Check inn cha Qatar Bw. Tajamul
Hussain kuhusu utalii wa Tanzania kwa ujumla.
Waziri
wa Biashara na Utalii wa Kenya Mh. Phylis Kandie akisakata rhumba na
Waziri wa Maliasili na utalii wa Tanzania Mh. Nyalandu katika banda la
Tanzania.
…………………………………………………………………..
Na: Geofrey Tengeneza – Berlin Ujerumani
Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu amekutana
na waziri mwenzake wa Biashara na Utaliiwa Kenya Bibi Phylis Kandie
katika banda la Kenya na kuwa na mazungumzo yanayohusu ushirikiano wa
nchi mbili katika sekta ya Utalii. Mazungumzo hayo hayakuwa rasmi hivyo
hayakuhudhuriwa na wandishi wa habari
Aidha Wiziri Nyalandu alitembelea banda la Tanzania na
kuzungumza na washiriki wa maonesho ya ITB kutoka makampuni mbalimbali
washiriki hao kwa ambapo amewapongeza kwa kuitangaza vema Tanzania
katika maonesho hayo.
EmoticonEmoticon