Na Veronica Simba
Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene amefanya ziara mkoani Lindi
na Mtwara mwanzoni mwa wiki kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya
Wizara yake ambapo aliahidi huduma za umeme na maji kwa wananchi
mbalimbali.
Akiwa
Madimba mkoani Mtwara, baada ya kupokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi
wa mtambo wa kuchakata gesi, Waziri Simbachawene alimwagiza Msimamizi
Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba kutoa huduma
ya maji safi kwa wananchi wanaozunguka maeneo hayo.
“Kutokana
na taarifa yenu, mtakuwa na hifadhi ya maji ya kutosha hapa. Pamoja na
matumizi yenu mbalimbali, hakikisheni mnatoa huduma ya maji kwa wananchi
wanaozunguka mtambo,” alisema Waziri.
Vilevile, Waziri Simbachawene alitoa ahadi ya umeme kwa Kijiji cha
Luvula kilichoko Msimbati. Alisema Kijiji hicho na vingine 15 vilivyo
jirani na Kiwanda cha kufua umeme cha Mnazibay, vitapatiwa umeme kabla
ya mwezi Oktoba mwaka huu.
“Tunaendelea
na zoezi la kusambaza umeme nchi nzima. Lengo letu ni kuhakikisha idadi
ya watanzania wanaopata umeme inaongezeka zaidi na zaidi ili kuwezesha
lengo la nchi yetu kufikia uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025
kama dira ya maendeleo inavyoonesha,” alisema.
Ziara
hiyo ya Waziri Simbachawene, ni ya kwanza kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara
tangu aliposhika wadhifa wa Uwaziri wa Nishati na Madini, Januari mwaka
huu.
Katibu
Tawala wa Mkoa wa Mtwara, Alfred Luanda (aliyesimama), akiwasilisha
taarifa fupi ya hali ya mmomonyoko wa ardhi uliosababisha mazingira ya
hatari kwa Kiwanda cha kuchakata gesi asilia cha Maurel & Prom
Tanzania (M&P), kilichopo Mnazi Bay – Mtwara. Wanaosikiliza ni
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa tatu kutoka
Kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (katikati), na baadhi
ya Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini walioongozana na Waziri.
Baadhi ya nyumba wanazoishi wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kutoka Kulia)
akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa
Madimba – Mtwara. Pamoja naye ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la
gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (Kushoto – sambamba na Waziri) na Mkuu
wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud
(Kulia kwa Waziri.
Msimamizi
Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba (kushoto),
akifafanua jambo kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene
(wa pili kutoka kushoto) wakati akikagua nyumba za wafanyakazi wa Mtambo
wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara.
Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene, akikagua sehemu ya Mtambo wa
kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara wakati wa ziara aliyoifanya
mwanzoni mwa wiki mkoani humo.
Matanki
ya kuhifadhia maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali, yaliyopo katika
eneo la Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba – Mtwara. Katika
ziara yake mtamboni hapo, Waziri wa Nishati na Madini, George
Simbachawene aliagiza maji hayo yatumike pia kuwasaidia wananchi
wanaoishi maeneo jirani.
Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha
ya pamoja na wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba –
Mtwara.
Msimamizi
Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam,
Mhandisi Kapuulya Musomba (wa pili kushoto) akimwonyesha kitu Waziri wa
Nishati na Madini, George Simbachawene wakati alipotembelea Mtambo wa
kuchakata gesi wa Madimba – Mtwara, mwanzoni mwa wiki.
Baadhi
ya Wafanyakazi/Vibarua katika Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa
Madimba – Mtwara, wakiendelea na kazi wakati Waziri wa Nishati na
Madini, George Simbachawene alipofanya ziara kukagua maendeleo ya Mradi
huo mwanzoni mwa wiki.
Sehemu ya Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba mkoani Mtwara.
Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene (katikati) akiwa katika picha
ya pamoja na wafanyakazi wa Mtambo wa kuchakata gesi asilia wa Madimba –
Mtwara wakati wa ziara yake Mtamboni hapo mwanzoni mwa wiki.
Waziri
wa Nishati na Madini, George Simbachawene (kulia) akijadili jambo na
mmoja wa wasimamizi wa Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba – Mtwara,
wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki kukagua maendeleo ya Mradi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Luvula, Msimbati mkoani Mtwara, Yusuf Haki
Yusuf (Kulia) akiwasilisha maombi ya wananchi wa Kijiji chake kupatiwa
umeme kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili
kushoto) wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki. Waziri aliahidi kuwa
Kijiji hicho na vingine 15 vilivyo jirani na MnaziBay vitapatiwa umeme
kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu. Kulia kwa Waziri, ni Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara, Halima Dendegu.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukamilisha ziara yake kukagua Mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba – Mtwara. Kulia kwa Waziri ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam, Mhandisi Kapuulya Musomba na kushoto kwa Waziri ni Mkuu wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (Kushoto), akisalimiana na Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Msimbati, Joha Matwili, alipowasili MnaziBay kujionea athari za mmonyoko wa ardhi uliotishia hali ya usalama wa mazingira ya Kampuni ya Tawel & Prom inayozalisha umeme unaotumiwa na wakazi wa Lindi na Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Hawa Dendegu (aliyenyoosha mkono), akimwonyesha Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, jinsi maji ya bahari yalivyoathiri eneola MnaziBay, karibu na kampuni ya kuzalisha umeme ya Maurel & Prom.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene, (aliyenyoosha mkono) akimwonyesha kitu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu (wa pili kulia) wakati Waziri alipotembelea eneo hilo kujionea athari za mmomonyoko wa ardhi uliotishia usalama wa mazingira ya Kampuni ya kufua umeme ya Maurel & Prom iliyo jirani na eneo hilo.
Athari ya mmomonyoko wa ardhi katika eneo la MnaziBay inavyoonekana
pichani. Mmomonyoko huo umetishia usalama wa Kiwanda cha kufua umeme
unaotumiwa na wakazi wa Lindi na Mtwara cha Maurel & Prom.
Meneja Uzalishaji na Uendeshaji wa Kampuni ya Maurel & Prom, David
Chajdronnier (katikati) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati na Madini,
George Simbachawene (Kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Hawa Dendegu
(Kulia) kuhusu mmomonyoko wa ardhi eneo la MnaziBay, Mtwara. Kampuni
hiyo ndiyo inazalisha umeme unaotumiwa na wakazi wa Mtwara na Lindi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Luvula, Msimbati mkoani Mtwara, Yusuf Haki Yusuf (Kulia) akiwasilisha maombi ya wananchi wa Kijiji chake kupatiwa umeme kwa Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene (wa pili kushoto) wakati wa ziara yake mwanzoni mwa wiki. Waziri aliahidi kuwa Kijiji hicho na vingine 15 vilivyo jirani na MnaziBay vitapatiwa umeme kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu. Kulia kwa Waziri, ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendegu.
Kisima cha gesi namba 3 kilichopo Msimbati, Mtwara. Kisima hiki hupokea gesi asilia kutoka Kisima namba 1 na Kisima namba 2, kisha kupelekwa Madimba kwenye mtambo wa kuchakata gesi hiyo.
Sehemu ya mtambo wa kisima cha gesi namba 3 kilichopo Msimbati, Mtwara ambacho hupokea gesi kutoka Visima namba 1 na 2, kisha kupelekwa Madimba katika mtambo wa kuchakata gesi.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akicheza mchezo wa ‘Pool Table’ katika ukumbi uliopo kwenye nyumba za wafanyakazi wa mtambo wa kuchakata gesi wa Madimba, Mtwara baada ya kuhitimisha ziara yake mwanzoni mwa wiki. Mahali hapo pa michezo ni maalum kwa wafanyakazi kwa ajili ya kujichangamsha baada ya kazi. Anayefuatilia mchezo huo ni Msaidizi wa Waziri, Mhandisi Joseph Kumburu.
Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene akikagua moja ya Valvu ya gesi, eneo la Somanga Fungu akiwa katika ziara yake mwanzoni mwa wiki kukagua miundombinu ya bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam. Wa kwanza Kulia ni Mkuu wa Mawasiliano Serikalini – Wizara ya Nishati na Madini na mwenye kofia nyeupe ni Msimamizi Mkuu wa Mradi wa Bomba la gesi, Mhandisi Kapuulya Musomba.
EmoticonEmoticon