Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimatafa Bernard Membe akitoa hotuba kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye alikuwa
Mgeni Rasmi katika sherehe ya mwaka mpya wa Kichina jana katika viwanja
vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Balozi wa China nchini Tanzania,
Dkt Lu Youqing akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimatafa Bernard Membe kutoa hotuba kwa niaba ya Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye alikuwa Mgeni
Rasmi katika sherehe ya mwaka mpya wa Kichina jana katika viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Balozi wa China nchini Tanzania,
Dkt Lu Youqing (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sadick Meck
Sadiki(kulia) wakicheza ngoma ya iliyoimbwa kwa lugha ya Kishwahili na
Kichina inayosema tupige jahazi iende mbali wakati wa sherehe ya mwaka
mpya wa Kichina iliyofanyika jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini
Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimatafa Bernard Membe akizugumza jambo na Balozi wa
China nchini Tanzania, Dkt Lu Youqing wakati wa sherehe ya mwaka mpya wa
Kichina iliyofanyika jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimatafa Bernard Membe(kushoto) na Balozi wa China nchini
Tanzania, Dkt Lu Youqing (katikati) wakati wa sherehe ya mwaka mpya wa
Kichina iliyofanyika jana katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es
salaam. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es SALAAM, Sadick Meck Sadiki.
Baadhi ya wageni waliaohudhuria
sherehe ya mwaka mpya wa Kichina iliyofanyika jana katika viwanja vya
Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
(Picha na Eleuteri mangi- MAELEZO)
………………………………………………………………………….
………………………………………………………………………….
Na Magreth Kinabo na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimatafa Bernard Membe,
ameipongeza Serikali Jamhuri ya China kwa msaada wake wa kuhakikisha
Tanzania imefungua idara ya maalum ya upasuaji wa moyo katika hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH).
Hayo yamesemwa na Waziri Membe jana katika viwanja vya Mnazi
Mmoja jijini Dar es salaam kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ambaye alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe
ya mwaka mpya wa Kichina.
“Tuna mengi ya kusema kuhusu misaada ya maendeleo inayoletwa na
ndugu zetu Wachina Sasa hivi muhimbili, kwa mfamo wametusaidia kufungua
idara maalum ya upasuaji wa moyo, ambayo sasa unaweza kufanya upasuaji
wa moyo jambo ambalo lilikuwa hadithi ya kufikirika katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania.
“Lakini sasa hivi Watanzania wanaweza kwenda kutibiwa ugonjwa wa
moyo kwa kupasua na kufanyiwa matibabu. Tunawapongeza Serikali ya China
kwa kuleta msaada mkubwa wa aina hii nchini Tanzania,” alisema Waziri
Membe.
Katika sherehe hizo za mwaka mpya,Jumuiya ya Wachina waishio
nchini Tanzania waliungana pamoja na wageni wengine kusherehekea siku
kuu hiyo, ambayo itaanza rasmi February 18, mwaka huu.
Waziri Membe akifafanua kuhusu mwaka huo, alisema kuwa
utajulikana kama mwaka wa kondoo, ambapo mwaka jana 2014 ulijulikana
kama mwaka wa farasi.
Jumuiya hiyo wamechagua siku hiyo ya Februari 14 kwa kuwa ni
mwisho wa wiki tofauti na siku yao rasmi ya mwaka mpya ambayo
itaangukuia Jumatano ambayo ni katikati ya wiki na kuwanyima wengine
fursa ya kuhudhuria na wanasherehekea siku yao ya mwaka mpya 2015.
Aliongeza misaada mingine ya maendeleo ilitolewa na nchi hiyo ni
miradi ya maji Dodoma na Chalinze mkoani Pwani, mradi ya kilimo Dakawa
mkoani Morogoro, Uwanja wa Taifa wa Michezo na Ukumbi wa mikutano wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, uliopo jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt Lu Youqing
alisema sherehe hiyo kama alama ya kufahamu utamaduni wa nchi hiyo,
imeshafanyika kwa mafanikio mkubwa kwa miaka sita nchini Tanzania na
inapendeza, ambayo ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili
katika sekta ya utamaduni.
“Uhusiano wa Tanzania na China
sasa uko katika kipindi kizuri cha Juu, mwaka 2014 uliopita ni miaka 50
ya uhusiano wa kidiplomasia baina ya Tanzania na China. Kwa nusu karne
uhusiano nchi hizi mbili zinasaidiana na urafiki wa baina ya nchi hizi
mbili umepata maendeleo makubwa,” alisema Balozi Dkt Youqing.
Balozi huyo aliishukuru Serikali Tanzania kwa kuunga mkono
sherehe hiyo na aliwaomba wananchi wa nchi hizo kushirikiana na
kusaidiana ili kupata maendeleo pande zote mbili.
Serikali hiyo ya China imepongezwa kwa kuwa nchi mfano wa kuigwa
kwa kutoa misaada mbalimbali Barani Afrika,ambapo imesaidia kutatua
migogoro na kutoa dola za Marekani milioni 35 kwa ajili ya kukabiliana
na ugonjwa wa ebola na kutoa madaktari 200 ili kukabiliana na janga hilo
katika nchi za Liberia,Guinea pamoja na Sierra Leone
EmoticonEmoticon