Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita akitoa hutuba fupi kwa mgeni rasmi.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya wasaidizi wa kisheria waliopatiwa mafunzo hayo.
Wanawake wa Wilaya ya Lushoto wakiwa kwenye sherehe hiyo ya uzinduzi wa mradi huo na ofisi.
Viongozi mbalimbali waliojumuika kwenye uzinduzi huo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita (mbele
katikati), akiwa katika picha ya pamoja na wasaidizi hao wa kisheria na
maofisa wa EfG.
Wanahabri
kutoka vyombo mbalimbali waliokuwepo kwenye uzinduzi huo. Kutoka
kushoto ni Shadrack (Channel 10), Nasra Abdallah (Tanzania Daima), Dotto
Mwaibale (Jambo Leo na Mtandao wa www.habari za jamii.com na Sophia kutoka Televisheni ya Mlimani.
Wanafunzi nao walijumuika kuona shughuli mbalimbali za uzinduzi huo hasa kikundi cha ngoma kilichokuwa kikitoa burudani.
Kikundi cha ngoma kikitoa burudani.
Zawadi zikitolewa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa EfG, Jane Magigita.
Mkurugenzi
Mtendaji wa EfG, Mary Magigita akiwa ameshika mkungu wa ndizi
aliozawadiwa. Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Lushoto, Josephine
Kisigila.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto, Dk.Hassan Shelukindo
(kushoto), akifurahi na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for
Growth (EfG), Jane Magigita baada ya kukabidhiwa machapisho mbalimbali
ya EfG.
………………………………………………………………………..
Doto Mwaibale
WAJASIRIAMALI
wanawake wametakiwa kutumia mafunzo ya usimamizi wa sheria katika
masoko waliyopata kwa kuwaelimisha wengine badala ya kukaa nyumbani bila
ya kutoa elimu hiyo.
Mwito
huo ulitolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto
Dk.Hassan Shelukindo wakati wa uzinduzi wa ofisi ya mradi wa msaada wa
kisheria kwa wafanyabiashara sokoni na ofisi ya mradi huo wilayani humo
mkoani Tanga jana kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmshauri hiyo Jumanne
Shauri.
“Ninyi
Wanawake wa Lushoto mmepata bahati kubwa ya kuletewa mradi huu pamoja
na mafunzo haya mliyopata nawaombeni nendeni mkayafanyie kazi katika
maeneo yenu” alisema Dk. Shelukindo
Alisema
elimu waliyoipata ya msaada wa kisheria ni muhimu sana kusaidia jamii
katika masoko na itasaidia kupunguza unyanyasaji wa kijisinsia.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), ambalo linaendesha
mradi huo, Jane Magigita alisema lengo la mradi huo katika wilaya hiyo
ni kuhamasisha na kulinda haki za wafanyabiashara iwanawake katika
masoko kwa kuwapatia elimu ya sheria, biashara, elimu ya vicoba, elimu
ya uongozi na usimamizi wa vikundi.
Alisema
EfG ni shirika la pekee nchini linalotoa msaada wa kisheria kwa sekta
isiyorasmi hivyo kuonesha ni kiasi gani sekta hiyo ilivyo sahulika.
Alisema
EfG inaendesha mradi huo katika masoko ya wilaya ya Lushoto pamoja na
vikundi mbalimbali vya maendeleo na kuwa shirika hilo linawajibika kutoa
mafunzo ya siku 25 kwa wasaidizi 25 ambao watasambaza huduma sheria
kwa jamii.
Alisema mafunzo hayo yanatolewa kwa awamu tano ambapo kila awamu yatakuwa yanafanyika kwa takribani siku tano.
”
Shirika linawajibika kutoa mafunzo mafunzo mbalimbali kwa
wafanyabiashara ikiwa na lengo la kuinua hali za wanawake
wafanyabiashara sokoni kupitia mafunzo ya biashara, uundwaji wa vikundi
vya Vicoba, mafunzo mbalimbali kwa watendaji na viongozi wa Halmshauri
ya wilaya ya Lushoto kwa lengo la kuboresha hali za wafanyabiashara
sokoni” alisema Magigita.
Alisema
mpaka sasa shirika hilo limefanikiwa kuwapatia mafunzo ya sheria ya
siku tano wasaidizi wa sheria 25, wanaume 8 na wanawake 17 kutoka katika
masoko na wengine kutoka katika vikundi vya maendeleo ndani ya
Halmshauri ya Wilaya ya Lushoto.
Alisema
pia wanakituo maalumu cha msaada wa sheria katika ofisi za EfG Lushoto
ambapo wafanyabiashara mbalimbali wanaruhusiwa kupeleka matatizo yao ya
kisheria kila siku za Jumatatu na Jumatano kuanzia saa tatu asubuhi
mpaka saa 10 jioni.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
EmoticonEmoticon