KINAA AANZA ZIARA TANGA LEO

January 04, 2015
KATIBU MKUU wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Abdurahamani Kinana anatarajiwa kuwasili mkoani Tanga leo kwa ajili ya kufanya ziara ya siku mbili mkoani Tanga  itakayoambatana na kuzungumza na wananachi kupitia mikutano ya hadhara katika maeneo ambayo atapita.


Akizungumza na MTANDAO HUU Ofisini kwake, Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga,Shijja Othumani alisema kuwa katibu huyo atapokelewa njia ya panda ya Segera na kuelekea wilayani Lushoto kwa ajili ya ziara ya kikazi.

Shija alisema kuwa ziara hiyo itafanyika kwenye Halmasahuri ya Bumbuli kwenye kiwanda cha Chai cha Mponde ikiwemo kuzungumza na wananchi wanaoishi maeneo mbalimbali kabla ya siku ya pili kuelekea wilaya ya Tanga mjini.

 Alisema kuwa siku ya pili katibu huyo atakuwa na mkutano wa hadhara utakaofanyika kwenye viwanja vya Tangamano jijini Tanga ambapo lengo la ziara hiyo ni kuwashukuru wakazi wa mkoa wa Tanga kwa kukipa ridhaa kwenye chaguzi wa serikali za mitaa kwenye uchaguzi uliofanyika Desemba mwaka jana.

Aidha alisema kwenye uchaguzi huo chama cha mapinduzi (CCM)
kilifanikiwa kupata ushindi wa asilimi 100 ambayo ni mafanikio makubwa ambapo kwa upande wa vijijini kilipata ushindi wa asilimia 95 na vitongoji walipata asilimia 97

Hata hiyo,Katibu huyo alitoa wito kwa viongozi waliochaguliwa kwenye chaguzi hizo kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao ipasavyo na kwa uadilifu ili kuweza kuchochea kasi ya maeneo kwa wananchi waliowap ridhaa ya kuwaongoza.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »