Mbunge
wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete(kushoto)
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa duka jipya la Vodacom Tanzania
lililopo Chalinze mjini Mkoa humo. Katikati ni Meneja Uhusiano wa Umma
wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu,(kulia)Mkuu wa Idara ya Uuzaji na
usambazaji bidhaa wa kampuni hiyo Upendo Richard. Hafla hiyo imefanyika
leo mkoani humo.
Mkuu
wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo
Richard(kulia)akimfafanulia jambo kuhusiana na simu aina ya Vodafone
smart kicka Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani
Kikwete (katikati) mara baada ya kuzindua duka jipya la Vodacom
Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa humo,Kushoto ni Meneja Uhusiano wa
Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete wapili kutoka
kulia ,akigonganisha glasi za mvinyo na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom
Tanzania ikiwa ni ishara ya kusherehekea uzinduzi wa duka jipya la
kampuni hiyo alilolizindua lililopo Chalinze mjini Mkoa humo. Hafla hiyo
imefanyika leo mkoani humo.
Mkuu
wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo
Richard(kushoto)akimfafanulia jambo Mbunge wa jimbo la Chalinze mkoani
Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete (kulia) alipofika kuzindua duka jipya la
Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa humo,Kulia kwa Mheshimiwa
ni Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu.
Duka jipya la Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini Mkoa wa Pwani.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete wanne toka
kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom
Tanzania,baada ya kuzindua duka jipya la kampuni hiyo lililopo Chalinze
mjini Mkoani humo.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani Mh. Ridhiwani Kikwete,ametoa ushauri
kwa Makampuni ya Mawasiliano kufungua zaidi vituo vya kutoa huduma
kwa wateja mkoani Pwani na maeneo mengine ya miji midogo inayokua kwa
kasi ili kuwawezesha wateja wake kupata huduma kwa karibu badala ya
kuzifuata mbali na kupoteza muda mwingi ambao wangeutumia kufanya
shughuli za uzalishaji.Alitoa ushauri huo wakati akifungua duka la
Vodacom Tanzania lililopo Chalinze mjini ambapo pia alitoa pongezi kwa
hatua hiyo.
Katika
kuhakikisha wakazi wa vitongoji vya Chalinze na maeneo jirani ya
Ruvu,Miono,Gwata wanapata huduma kwa karibu,Kampuni ya mawasiliano ya
Vodacom Tanzania leo imefungua duka jipya katika eneo la Chalinze.
Chalinze
ni moja ya kituo maarufu katika mkoa wa Pwani ambacho wanapitia
wasafiri wengi wanaotumia barabara ya Morogoro pia ni makutano ya
barabara ya kuelekea mikoa ya Kaskazini ya Moshi,Tanga na
Arusha.Vilevile mji huu unakuwa kwa kasi kutokana na kuongezeka kwa
wafanyabiashara wanaowekeza eneo hili.
Duka
hili jipya lenye mazingira rafiki kwa wateja litakuwa linatoa huduma
mbalimbali kwa wateja wa Vodacom ikiwemo huduma kwa mawakala wa M Pesa
na uuzaji wa bidhaa za Vodacom na litawawezesha wateja wa Chalinze na
vitongoji vyake wakiwemo wasafiri wanaoelekea mikoa mballimbali na
nje ya nchi kupata huduma bora.Mtandao wa Vodacom unaongoza kwa
kupatikana vizuri na umeenea sehemu zote katika mkoa wa Pwani.
Mkuu
wa Idara ya Uuzaji na usambazaji bidhaa wa Vodacom Tanzania Upendo
Richard wa Vodacom Tanzania, alisema ufunguzi wa duka hili la kisasa
ni mwendelezo wa malengo ya Vodacom kuendeleza kuboresha maisha murua
kwa kila mtanzania kwa kupata huduma za kampuni hiyo zenye ubora na
kuwafikia wateja kwa urahisi zaidi popote pale walipo ikiwemo huduma
mpya ya kilimo klabu inayolenga kuwawezesha wakulima nchini.
“Uzoefu
na utafiti umetuonyesha kuwa wananchi wanataka ubora,kama mtandao
unaoongoza nchini tumejizatiti kuhakikisha tunafanya ubunifu wa hali ya
juu wa kiteknolojia ili kutumia mtandao wa simu kuboresha maisha ya
wananchi ikiwemo kutoa huduma bora na ndio maana tunazidi kufungua
maduka kama haya kwa ajili ya kuwasogezea karibu wananchi huduma bora,na
ninawahakikishia kuwa popote wateja wetu walipo tutawafikia na
tunawashukuru sana wateja wetu kwa kutuunga mkono na tunawakaribisha
ambao hawajajiunga na familia ya Vodacom kujiunga na kupata huduma bora
kwa gharama nafuu.”Anasema Richard
Vodacom
ina mtandao wa maduka 85 na wakala mbalimbali wakuuza bidhaa zake
nchini na duka lililofunguliwa leo ni la 3 kufunguliwa katika mkoa wa
pwani
EmoticonEmoticon