KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA JANA KILILAZIMIKA KUAHIRISHWA BAADA YA MADIWANI KUPITIA CHAMA CHA WANANCHI CUF KUGOMA KUJIORODHESHA

September 25, 2014

 Kikao cha Baraza  la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga jana kililazimika kuahirishwa baada ya  madiwani kupitia Chama cha Wananchi CUF kugoma kujiorodhesha wakipinga kitendo cha aliyekuwa diwani wa kata ya Marungu  kupitia chama chao na baadaye kuhamia CCM,Mohamed Mambeya kushiriki..

Mambeya alihamia CCM mwezi uliopita na kukabidhiwa kadi ya CCM na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Taifa,Abdallah Bulembo katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Tangamano.

Kikao hicho ambacho kilikuwa maalumu kwa ajili ya kupokea taarifa ya mkaguzi wa hesabu za Serikali (CAG),hakikuweza kufanyika kutokana na akidi ya wajumbe kushindwa kufikia theluthi tatu  ya madiwani 35 wa Halmashauri hiyo.

Waliojisajili katika daftari la mahudhurio katika baraza hilo ni
madiwani 21 pekee wa CCM lakini wenzao wa CUF waliingia na kuketi kwenye viti bila kujiorodhesha kwenye daftari  .

Licha ya Meya wa Jiji la Tanga,Omari Guledi kuwasihi wajiandikishe katika daftari hilo ili kikao kianze lakini madiwani hao wa CUF walikaa kimya huku nje ya jengo la Halmashauri hiyo kukiwa na ulinzi wa askari wa kikosi cha kuliza ghasia .

Baada ya kusubiri wa kwa saa moja, ndipo Meya akatangaza kuahirisha kikao hicho na kutoa sababu kwamba akidi haikutumia .

Akizungumza mara baada ya kuahirisha kikao hicho ,Diwani wa kata ya Mwanzange kupitia CUF ambaye pia ni Mwenyekiti wa c
Hama hicho Wilaya ya Tanga,Rashid Jumbe alisema wamelazimika kugomea kikao hicho kupinga kitendo cha Mambea kushiriki hali akijua kuwa si mjumbe halali kwa sababu amehama CUF.

“Mambeya anaruhusiwa kushiriki kikao cha baraza la madiwani
kumwakilisha nani wakati amejivua uanachama wa CUF iliyompa tiketi ya kuwa diwani wa kata ya Marungu?kama wanataka ashiriki waitishe uchaguzi agombee akichaguliwa kupitia CCM hatutakuwa na nongwa tena”alisema Jumbe.

Meya wa Jiji la Tanga,Guledi aliifahamisha Mwananchi kwamba
amelazimika kuahirisha kikao hicho kutokana na akidi kutotimia na kwamba ataitisha tena kikao hicho baada ya kujipanga upya.

Alisema kikao hicho kilikuwa na lengo la kupokea taarifa ya CAG na baada ya hapo kumuwezesha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga kutangaza kama imepata hati safi na kwa vigezo vipi.

Kuhusu tuhuma za kumruhusu Mambeya kushiriki kikao hicho,Meya huyo alisema tatizo bado liko kwa uongozi wa CUF kwa sababu bado hawajawasilisha kwake  barua ya kumtaarifu juu ya kuhama kwake katika chama chao.

Akizungumza na Mwananchi mara baada ya kuahirisha kikao hicho ,Diwani wa kata ya Mwanzange kupitia CUF ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya ya Tanga,Rashid Jumbe alisema wamelazimika kugomea kikao hicho kupinga kitendo cha Mambeya kushiriki hali akijua kuwa si mjumbe halali kwa sababu amehama CUF.

“Mambeya anaruhusiwa kushiriki kikao cha baraza la madiwani
kumwakilisha nani wakati amejivua uanachama wa CUF iliyompa tiketi ya kuwa diwani wa kata ya Marungu?kama wanataka ashiriki waitishe uchaguzi agombee akichaguliwa kupitia CCM hatutakuwa na nongwa tena”alisema Jumbe.

Kuhusu barua,Mwenyekiti huyo alisema CUF ilishamwandikia Mkurugenzi wa Jiji la Tanga,Juliana Malange  ikiamini kuwa ndiye Mtendaji.

“Kama utaratibu ni kumwandikia Meya basi leo hii,tunamwandikia na kumpelekea,ila wafahamu kuwa wanachifanya ni ujanja ambao  hauna maana kwa maendeleo ya wananchi na watambue kama ataendelea kushiriki hatutakoma kufanya mgomo”alisema Jumbe.

Mwenyekiti huyo alisema CUF inaandaa maandamano makubwa yatakayoonyesha jinsi wananchi wasivyoridhishwa na kitendo cha uongozi wa Halmashauri unavyovunja sheria lakini pia CUF itaeleza jinsi fedha zinavyofujwa kupitia Mambea.

Wananchi jijini hapa jana walikuwa katika hofu kwamba ingetokea vurugu katika kikoa hicho kutokana na msimamo uliokuwa umetangazwa na CUF kwamba walikuwa tayari kuuawa na askari polisi kuliko kumwacha Mambeya ahudhurie kikao hicho.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »