NSSF WAUSHAURIWA KUANZISHA MFUKO MAALUM WA KUWASOMESHA WATOTO WANAOZALIWA NJE YA NDOA

May 18, 2014

Social-Security-Fund-NSSF(1)(1)MFUKO  wa hifadhi ya jamii( NSSF) umeshauriwa  kuanzisha mfuko maalum  wa kuwasaidia watoto wanaozaliwa nje ya ndoa kwa kuwa hadi sasa mfuko huo unatoa mafao kwa watoto walioko ndani ya ndoa huku wanaozaliwa nje wakiwa hawapati mafao kutokana na kutelekezwa na baba zao.
Aidha kwa kipindi hiki cha miaka 50 toka kuanzishwa kwa mfuko kuna wanachama wengi wenye watoto wengi walioko ndani ya ndoa na nje ya ndoa huku watoto hao wan je wakiwa wanaachwa wakiteseka pamoja na mamazao.
Akizungumza jana mara baada ya kumalizika kwa mkutano mkuu wa mfuko huo  uliokuwa ukifanyika mjini hapa mratibu wa dangote Esta Baruti alisema kuwa watoto wengi walioko nje ya ndoa hawapatiwi mafao hivyo ni vema mfuko huo ukaangalia namna ya kusaidia watoto hao.
 Alieleza kuwa wanachama wengii wa mfuko huo wana  watoto walioko ndani ya ndoa na nje ya ndoa na kwamba wanaopatiwa mafao ni wale tu walioko ndani ya ndoa jambo linalowafanya watoto hao wan je kukosa haki zao za msingi kama elimu na mengineo.
Alifafanua kuwa watoto hao wan je wanaponyimwa mafao kwa kuwa wamezaliwa nje kunawaathiri kisaikolojia kwa kuwa wao hawana  makosa na  sio wao waliochagua kuzaliwa na wazazi walioko nje ya ndoa.
“mimi nilishaona sana hili tatizo ni kubwa sana na hasa kwa akina mama wanaoachiwa wale watoto kwa kuwa baba zao hawawashirikishi mafao yao kwa hawa bali ni wale tu watoto wao walioko ndani  ya nyumba zao hili jambo naomba lifikiriwe sana na huu mfuko”aliongeza Baruti.
Aidha alieleza kuwa ni vema mfuko huo ukafikiria namna ya kuwasaida watoto hao pamoja na wakina mama kwa kuwatafutia njia mbadala  kwa kuwa wao ndio wanaobaki njia panda bila kujua wawafanyeje hao watoto hao na hivyo kuwafanya waishi katika mazingira magumu.
Wakati huo huo baadhi ya wadau wa mfuko huo waliutaka mfuko huo kuangalia maeneo ya kuwekeza maabara haswa katika shule za kata ili kuwasaidia wanafunzi kupata tekenolojia mbali mbali.
Mmoja wa wadau hao Said Habibu alisema kuwa mfuko huo umekuwa ukisaidia jamii sana hasa kati ka uwekazaji na hivyo endapo utawekaza zaidi katika maabara kwa shule za kata kutasaidia sana taifa kupata wanasanyansi wengi kwani shule za kata zina upungufu mkubwa wa maabara jambo linalowanyima wanafunzi kujifunza kwa vitendo.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »