NI MCHEZAJI WA BARCELONA ALIYERUSHIWA NDIZI NA KISHA AKAIOKOTA NA KUIMENYA NA KISHA KUILA.
Baadhi
ya wahariri na waandishi wa Habari wa Magazeti ya Mtanzania, Bingwa,
Dimba, Rai na The African, Mwani Nyangasa na wenzake wakila Ndizi kwa
pamoja kama ishara ya kumuunga mkono mchezaji wa Barcelona Daniwl Alves,
ambaye ni Mwafrika aliyeonyeshwa vitendo vya ubaguzi wa rangi hivi juzi
wakati akiwa mchezoni na timu yake ilipokuwa ikicheza na Villarreal ya
Hispania, ambao mashabiki walimrushia ndizi mbivu uwanjani wakimaanisha
kumfananisha na Nyani na yeye kwa kuwaonyesha kuwa hajali kitendo hicho
aliiokota na kuimenya na kisha kuanza kuila, jambo ambalo liliungwa
mkono na wengi na kumpongeza kwa kitendo chake cha ujasiri, na kuendelea
na mchezo.
Baloteli
pia ni mmoja kati ya wachezaji Waafrika aliyeunga mkono kitendo cha
mwafrika mwenzake kuwakebehi na kuwadharau mashabiki hao wa ubaguzi. Na
pia Baloteli ni mmoja kati ya wachezaji wanaokumbana na vitendo hivyo
vya unyanyasaji uwanjani mara kwa mara.




EmoticonEmoticon