MIMI Hafidh
Athumani Kido, nikiwa na akili timamu natangaza kutojihusisha na shughuli zote
za Coastal Union, hasa usemaji wa klabu.
Miongoni mwa
sababu nyingi zilizonifanya kutangaza uamuzi huo ni sintofahamu iliyozuka ndani
ya klabu yetu, kwa taaluma yangu ya uandishi wa habari lazima niwe na msimamo
juu ya mambo yanayoendelea kwenye jamii.
Ili
niendelee kufanya kazi na klabu hii kwa wakati huu wa misuguano, lazima niwe na
upande; kwa maana upande unaounga mkono uongozi ama upande usiokuwa na Imani na
uongozi. Lakini mimi nimeamua kutounga mkono upande wowote.
Kwa hivyo
basi, ili niwe katika mstari sahihi nimeamua kukaa pembeni nifanye shughuli
zangu za uanahabari kwa furaha na amani.
Bado ni
mwanachama halali wa Coastal Union Sports Club, namba yangu ya kadi ni 0013.
Nitaendelea kutoa ushauri na kuishabikia klabu yangu ambayo nimekuwa nikimuona
marehemu baba yangu na kaka zangu wakiishabikia tangu nikiwa mdogo.
EmoticonEmoticon