*ZIARA YA KINANA TEMEKE, AKUTANA NA VIKUNDI VYA VICOBA VILIVYOASISIWA NA MTEMVU
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Kigamboni Dk.
Faustine Ndungulile, alipowasili kwenye Ofisi ya CCM wilaya ya Temeke
kwa ajili ya kuanza ziara katika wilaya hiyo leo ikiwa ni siku ya pili
ya ziara yake ya siku nne mkoani Dar es Salaam. Wapili ni Mbunge wa
Temeke Abbas Mtemvu.
Kinana
akitoka katika ofisi ya CCM wilaya ya Temeke baada ya kuzungumza na
Kamati ya Siasa ya Wilaya hiyo, Wapili ni Mtemvu na kulia ni Mkt CCM
Dsm, Ramadhani Madabida
Kinana
na Madabida wakiwa katika bodaboda ya mwanachama wa VICOBA wakati
Kinana, alipokuwa akienda kwenye mkutano wake na Vicoba Temeke katika
ukumbi wa Kata ya 15 Pub, Temeke. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Mtemvu katika bodaboda wakati wa kwenda kwenye kikao hicho na Vicoba wa Temeke
Kinana
akishuka katika bodaboda baada ya kufika kwenye ukumbi wa Kata ya 15
Pub, kwenye mkutano na Vicoba Temeke. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Dar es Salaam. Ramadhani Maadabiba.
Kinana akiingia ukumbini na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Temeke Yahya Sikunjema kwa ajili ya kuzungumza na Vicoba wa Temeke
Vicoba wakimshangilia Kinana alipozungumza nao katika ukumbi wa Kata ya 15 Pub, Temeke
Msanii wa Machozi Theatre Group, akionyesha machejo Kinana alipokutana na Vicoba, Temeke
Mtemvu
akimtuza msanii wa kikundi cha Machozi Theatre Group kikundi hicho
kilipotumbuiza wakati Kinana kizungumza na Vicoba wa Temeke katika
ukumbi wa Kata ya 15 Pub.
Maliki Ndembo (65) akisoma gazeti la Uhuru nje ya ukumbi wa Kata ya 15, Temeka
Kinana
akikagua mitambo ya mradi uliokuwa wa kusafisha gesi kutoka kwenye taka
eneo la Mtoni, Temeke. Mradi wenye mitambo hiyo uliopo chini ya Jiji la
Dar es Salaam, haukuwahi kufanya kazi hadi sasa na sasa Halmashauri ya
wilaya ya Temeke inataka uwe chini ya miliki yake ili iweze kuundeleza.
Kinana
akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick baada ya
kukagua eneo la mradi huo. Picha zote na Bashir Nkoromo
*******************************
KINANA ALIPOWATEKA WANAKIGAMBONI, MGOGORO KUHUSU UJENZI MJI WA KISASA ENEO HILO AAHIDI KUUPELEKA VIKAO VYA NGAZI ZA JUU CCM
*******************************
KINANA ALIPOWATEKA WANAKIGAMBONI, MGOGORO KUHUSU UJENZI MJI WA KISASA ENEO HILO AAHIDI KUUPELEKA VIKAO VYA NGAZI ZA JUU CCM
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano
wa hadhara uliofanyika jana, Machi 26, mwaka huu, katika eneo la
Kigamboni, wiulayani Temeke akiwa katika ziara yake mkoani Dar es
Salaam, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua
na kugagua utekelezaji wa ilani ya Chama.
Akizungumza na wananchi wa
Kigamboni, Kinana ameahidi kulichukua suala linaloonekana kuzua mgogoro
mkubwa baina ya wananchi na serikali la ujenzi wa mji wa kisasa wa
Kigamboni, Kinana ameahidi kulifikisha kwenye vikao vya ngazi ya juu
kabisa vya CCM kwa uamuzi wa uhakika na wa kudumu.
Kinana amesema, baada ya
kulifikisha kwenye vikao vya juu ya CCM atarejea tena Kigamboni
kuzungumza na wananchi ili kuwapa majibu sahihi.
"Hapa
ni lazima tujue, wazo la kubuniwa mradi huu lilianzishwa na nani, kwa
lengo na maslahi gani, na wananchi ninyi mnaoishi hapa mlihusishwa kwa
kiwango gani kuhakikisha mchakato mzima unakuwa halali kwa mujibu wa
sheria za nchi", alisema Kinana.
Maelfu ya wananchi wakimsikiliza Kinana alipoowahurubia katia mkutano huo
Kassim Abdallah mkazi wa Vijibweni Kigamboni akitoa hoja zake mbele ya Kinana kuhusu mradi huo
Khalfan
Iddi ambaye alikuwa kada wa CUF akikabidhi kadi yake kwa Kinana baada
ya kuridhiwa na hotuba ya katibu mkuu huyo kwenye mkutano huo wa
Kigamboni
Kinana akiagana na wananchi baada ya mkutano
Kinana akiongdoka uwanjani baada ya mkutano. Kulia ni mwenyekiti wa CCM Temeke, Yahya Sikunjema.
EmoticonEmoticon