Katibu Mkuu Kiongozi,Balozi Ombeni Sefue.akitangaza baraza la mwaziri leo.
- Hakuna Mabadiliko Ofisi ya Rais
- Ofisi ya Makamu Wa Rais - Naibu Waziri Kitwanga amehamishwa na nafasi yake imejazwa na Mhe. Ali Mwalimu
- Mwigulu Nchemba amekuwa Naibu Wizara ya Fedha (Sera). Aliyekuwa nafasi hiyo sasa ni Waziri Kamili
- Uchumi na Mapato sasa anatoka Janet Mbene na inajazwa na Adam Malima
- Dr. Asha rose Migiro sasa ni Waziri wa Katiba na Sheria
- Kwenye Ulinzi na Kujenga Taifa ni Dr. Hussein Mwinyi
- katika Mambo ya Ndani - Mathias Chikawe
- Afya na Ustawi wa Jamii - Naibu wake sasa ni Waziri Kamili; naibu wa sasa ni Dr. Kebwe S. Kebwe
- Waziri Mulugo amepigwa chini rasmi . Nafasi yake imejazwa na Jenista Muhagama
- D. Sophia Simba amebaki na naibu wake akiwa ni Pindi chana katika wizara ya Jinsia na watoto.
- Katika wizara ya Mifugo na Maendeleo yake ni Dr. Titus Kamani mbunge wa Busega atakuwa Waziri mpya. Naibu wake ni Saning'o Kaika Telele na hivyo Wizara nzima imepata mawaziri wapya
- Mhe. Ole Medeye Amepigwa chini na nafasi yake kuchukuliwa na George Simbachawene katika wizara ya Ardhi ila bado waziri wake ni Prof. Tibaijuka)
- katika kilimo na Chakula waziri ni yule yule na Naibu wake ni Godfrey Zambi.
- Wizara ya Habari na michezo waziri ni yule yule Dr. Fenella Mukangara ila naibu wake ni mpya , Mtangzaji wa zamani na mbunge wa Singida Bw. Juma Nkamia.
- Maliasili na Utalii Nyalandu amekuwa Waziri Kamili. Naibu ni Mahmood Hassan Mgimwa
- Katika Nishati na Madini ni Prof. Sospeter Muhongo na Naibu wake ni Charles Kitwagwa akiichukua toka kwa Simbachawene.
EmoticonEmoticon