Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,
akifungua pazia kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo jipya la Kiwanda cha
Uchapaji Zanzibar na Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, huko
Maruhubi Mjini Unguja, ikiwa ni katika shamra shamra za Miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar,(kulia) ni Waziri Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais
Mohamed Aboud Mohamed.
Mkurugenzi
Mkuu wa Idara ya Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Dr. Aboud Sheikh Rajab,
akitoa maelezo kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) alipotembelea jengo jipya la
kiwanda cha uchapaji, Maruhubi jana,ikiwa ni shamra shamra za Mapinduzi
Matukufu ya Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,(kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya
Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Dr. Aboud Sheikh Rajab,kuhusu mashine mpya
zilizonunuliwa na idara ya uchapaji,wakati alipotembelea kuangalia
mashine kuona utendaji wake kazi,baada ya
kufanya unguzi rasmi,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,(kushoto) akiuliza suala kwa Mkurugenzi Kanda wa Kampuni ya MFI
DOCUMENT SOLUTION LTD, Rama Subramanian,ikiwa ndio wataalam wa mshine za
uchapishaji,alipotembela na kuona zinavyofanyakazi,wakati wa ufunguzi
wa jengo jipya la kiwanda hicho,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya
Mapinduzi ya Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed
Shein,(katikati) akipata maelezo kutoka kwa mtaalam wa mashine ya
CTP,ambayo inatoa picha kwa kutumia Plat,Mohamed Abass Rajab,(wa tatu
kushoto) wakati wa ufunguzi wa jengo jipya la kiwanda cha Uchapaji cha
Zanzibar jana,ikiwa ni shamra shamra za Miaka 50 ya Mapinduzi ya
Zanzibar. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
Imewekwa leo desemba 30 saa 06:24 jioni.
EmoticonEmoticon