Kocha wa makipa wa klabu ya Simba,James Kisaka aliyefariki dunia juzi katika Hospitali ya Burhani Jijini Dar es salaam na mwili wake kusafirishwa kijijini kwake Lusanga Wilaya ya Muheza hatimaye alizikwa leo katika makaburi ya familia yake.
Misa
ya mazishi ya Kocha huyo yaliyohudhuriwa na waombolezaji wengi
iliendeshwa na Padri wa Kanisa Anglikana Lusanga,Aidano Kamote.
Padri huyo aliwataka wapenzi wa michezo kuuchukulia msiba huo kama funzo la kutomsahau Mungu katika shughuli zao badala yake waimarishe ibada wakijua kuwa kuna siku uhai hautakuwepo tena.
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Simba,Said Pamba ambaye aliwakilisha viongozi na wachezaji wa Simba alisema klabu yake imempoteza kocha ambaye pengo lake si rahisi kuzibwa na mtu mwingine.
“James Kisaka alikuwa na mapenzi ya dhati na simba,tulikuwa tukimtegemea kwa ushauri na hata uzoefu wake ulisadia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya Simba”alisema Pamba .
Viongozi wengine waliohudhuria mazishi hayo ni Kamishna wa tume ya uchaguzi namdau maarufu wa michezo,Jaji John Mkwawa ambaye alisema alimfahamu Kisaka siku nyingi.
EmoticonEmoticon