BOSI TRBA ATAKA UMAKAMU WA RAIS TBF.

December 23, 2013
IMEWEKWA DESEMBA 23
 Na Oscar Assenga,Tanga.
MWENYEKITI wa Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Tanga(TRBA)Hamisi Jaffary amejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Umakamu wa Rais wa Shirikisho la mpira wa Kikapu nchini (TBF) unaotarajiwa kufanyika Desemba 29 mwaka huu.

Akizungumza jana,Jaffary alisema ameamua kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo kwa lengo la kuleta mabadiliko kwenye mchezo huo kwenye mikoa mbalimbali hapa nchini.

Alisema endapo atafanikiwa katika nafasi hiyo atahakikisha anajitahidi kuutoa mchezo huo hatua moja kwenda nyengine pamoja na kufanya uhamasishaji wa kuanzishwa mashindano ya kikapu ngazi ya mikoa na wilaya.

   "Nimechukua fomu hii kwa nia na madhumuni ya kuhakikisha tunafanya mabadiliko makubwa kwenye tasnia ya mchezo wa kikapu hapa nchni "Alisema Jaffary.

Aidha alihaidi kushirikiana na wenyeviti wa mikoa wa mchezo huo kuhakikisha wanaufikia malengo makubwa kwa kurudisha hamasa yake kwa kuanzisha mashindano mara kwa mara.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »