WANACHAMA WA CHAMA HICHO MKOANI TANGA WAKIMSIKILIZA KATIBU WA KANDA YA KASKAZINI,AMANI GOLUGWA AMBAYE HAYUPO PICHANI LEO |
KATIBU WA CHADEMA KANDA YA KASKAZINI,AMANI GOLUGWA AKISISITIZA JAMBO LEO. |
CHAMA cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema)kimesema kuwa licha ya kuwepo msuguano wa ndani lakini
kimetamba kuwa kitachukua kata zote sita zilizopo kanda ya kaskazini katika
uchaguzi utakaofanyika hivi karibuni hapa nchini.
Uchaguzi huo wa marudio unatokana na kata za Kiomoni,Mtae mkoani Tanga na Sombetini mkoani Arusha,Kiborolioni mkoani Kilimanjaro na Karachimbi Kiteto mkoani Manyara kutokuwa na madiwani wake kutokana na baadhi yao kujiuzulu na wengine kufariki dunia.
Tambo hizo zilitolewa na Katibu
wa Chadema Kanda ya Kaskazini,Amani Golugwa wakati akizungumza na viongozi wa
chama hicho mkoani hapa kwenye mafunzo ya Chadema ni msingi ambayo yalikuwa na
lengo la kuwajengea uwezo pamoja na kukabidhi vifaa vya awali vya kampeni kwa
kata zinazokabiliwa na uchaguzi huo ambazo ni Kiomoni na Mtae
Golugwa alisema vifaa hivyo vimetolewa kwa awamu ambapo awamu ya pili watakabidhi pikipiki ili viongozi wa chama hicho waweze kutimiza wajibu wao ipasavyo na hatimaye kuweza kupata ushindi kwenye chaguzi hizo.
Alisema chama hicho kitaingia
kwenye mchakato huo kwa kuangalia wanachama ambao watakao kuwa na uwezo wa
kuipeperusha bendera yao
kwa kuweka wagombea wanaokubalika kwa wananchi kwenye kata zao.
Katibu huyo alisema kuelekea
kwenye mchakato huo aliwataka wanachama kuwa na mshikamano wa dhata ambao
utakiwezesha chama hicho kupata ushindi na kuacha kutengeneza makundi yasiyo na
tija.
“Tunataka kutengeneza historia kwa madiwani
wawili kwenye jimbo la Tanga na kata nyingine zilizopo mikoa ya kanda ya kaskazini
“Alisema Golugwa.
Akizungumzia mafunzo
hayo,Golugwa alisema mafunzo hayo ya siku mbili yana lengo la kuwajengea uwezo
wanachama wake mkoani Tanga pamoja na kukiimarisha chama hicho kuelekea
uchaguzi ujao.
Waliopokea vifaa hivyo ni
Mwanamtama Bakari ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema kitongoji cha Luande kata ya
Kiomoni Jimbo la Tanga na Edward Ngereza wa Kata ya Mtae Jimbo Mlalo wilayani
Lushoto
EmoticonEmoticon