ADC KANDA YA KASKAZINI WACHAGUA VIONGOZI WA KUKIWAKILISHA MKUTANO MKUU TAIFA.

September 16, 2013
Burhani Yakub,Tanga.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha Alliance Democratic Change(ADC) Kanda ya Kaskazini,jana kilifanya uchaguzi na kuwapata wajumbe 10 watakaoiwakilisha  mikoa yao kutano mkuu wa chama hicho Taifa.

Waliochaguliwa katika mkutano huo uliokuwa na ushindani mkubwa ni Doyo Hassan Doyo,Mohamed Siyu, Mwarami Zimbwe,Asia Mgaza,Jamal Ally, Asha Juma, Rehema
Mhando, Rashid Hamza ,Zainab Juma na Hamida Msumeno.

Mkutano huo wa uchaguzi huo uliosimamiwa chini ya uongozi wa AyubMussa Kimangale kutoka tume ya uchaguzi ya Chama hicho ambapo ulifunguliwa na Mwenyekiti wa Taifa wa ADC,said Miraji Abdallah.

Akizungumza wakati akifungua mkutano huo uliofanyika Jijini
Tanga,Miraji aliwataka wajumbe kuwachagua viongozi ambao watamudu mikikimikiki ya chaguzi za Serikali ukiwamo wa Serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Alisema ADC licha ya uchanga wake lakini kimeundwa ili kuchukua madaraka ya Serikali na kimejidhatiti kwa hilo kutokana na ukweli kwamba kimeenea nchi nzima katika kipindi kifupi tangu kuundwa hivyo kinahitaji viongozi watakaojitoa ipasavyo.

“Hatutaki ADC kiwe ni chama chenye viongozi wa huku mikoani wa kushiriki makongamano au Semina,wala kuwa chama cha mkobani au magazetini,tunataka kuchukua uongozi wan chi”alisema Miraji.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »